habari


Ujezi wa Makazi Mapya ya Familia ya Mtoto Anthony Petro wa Ngara.

Ujenzi wa Nyumba ya Familia ya Mzee petro Magogwa ambaye ni Baba mzazi wa Mtoto Anthony Petro wa Kijiji Ngundusi ,Kata ya Kabanga wilayani Ngara mkoani Kagera ukiendelea katika kijiji hicho baada ya Wafadhili mbalimbali kujitokeza kuisaidia familia hiyo.

Ujenzi huo unafanyika katika eneo jipya jirani na Kabanga mjini ambapo ujenzi huo umefikia hatua hii Pichani.

Picha Na Shaaban Ndyamukama -Radio Kwizera Ngara.

Ujenzi huo unafanyika katika eneo jipya jirani na Kabanga mjini ambapo ujenzi huo umefikia hatua hii Pichani.

Hii ni nyumba ya awali ya Familia ya Mzee Petro Magogwa ambaye ni Baba mzazi wa Mtoto Anthony Petro wa Kijiji Ngundusi ,Kata ya Kabanga wilayani Ngara mkoani Kagera  akiifanyia ukarabati wakati huu akisubiri kupatiwa Makazi Mapya ya Kuishi.

Anaeonekana ni Dada Yake na Anthony, aitwaye Editha Petro ambaye amebaki kama muangalizi wa Familia baada ya Mtoto Anthony kuwa Masomoni Mkoani Kilimanjaro.

Picha Na Shaaban Ndyamukama -Radio Kwizera Ngara.


Post a Comment