habari Mpya


Uchafu wa Choo watishia Afya za Wafanyabiashara wa Soko la Nyankumbu Geita.

Baadhi ya Wafanyabiashara katika Soko la Nyankumbu mkoa wa Geita wako hatarini kukumbwa na Magonjwa ya mlipuko kutokana na Choo cha soko hilo kujaa na kutiririsha maji kwenye bwawa linalotumika kuoshea bidhaa zao hasa mboga mboga na viazi.

Habari Na Gibson Mika -Radio Kwizera Geita.

Wakizungumza na radio kwizera sokoni hapo, baadhi ya wafanyabiashara Bi Lidia Deus na Devota Afready wamesema kutokana na harufu mbaya inayotokana na choo hicho imeathiri biashara zao za migahawa kutokana na wateja wao kuhofia kupata magonjwa ya mlipuko.

Uchafu wa choo hicho.

Pia wameiomba Serikali kuwarekebishia miundombinu ya choo hicho ili kuepuka magonjwa ya mlipuko ambayo yanaweza kujitokeza na kusababisha kufungiwa kwa biashara zao.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mji wa Geita Bw. Modest Aprinali amesema Serikali ipo kwenye mchakato wa kupunguza uchafu katika soko hilo na kwamba jitihada za haraka zinafanyika katika kuchimba shimo jingine kutokana na shimo hilo kujengwa kwenye mkondo wa maji hali inayosababisha kujaaa kwa haraka pale mvua inaponyesha.

Post a Comment

0 Comments