habari Mpya


Tembo Wafanya Uharibifu wa Mazao Kata ya Kasulo,wilayani Ngara.

Tembo wakila .Picha na Maktaba Yetu. 

Tembo Wapatao 25 wakitokea katika Msitu wa Hifadhi wa Kimisi,mkoani Kagera  wamevamia kitongoji cha Kamuli, Kata ya Kasulo wilayani Ngara Mei 10, 2018, na kuharibu mazao ambayo thamani yake haijajulikana bado.

Akiongea kwa njia ya simu Afisa Mtendaji wa Kata ya Kasulo Bw. Peter Jeremiah Kapalala, amesema Tembo hao walivamia mashamba usiku wa kuamukia Alhamisi, na kuharibu mashamba ya Mahindi, Karanga na Maharage.

Wananchi wamejitahidi kuwafukuza tembo hao, ili warejeetena katika pori la hifadhi, lakini imetuchukua muda mrefu, kwani hadi saa tano asubuhi walikuwa bado wamo mashambani.” Alisema Mtendaji Kapalala.

Insemekana wanyama hao hawakuwadhuru watu na wala watu hawakuwadhuru tembo hao, na kwamba pamoja na kuwafukuza inaonekana wanyama hao hawakwendambali, na wananchi wana wasiwasi kwamba uenda wakarejea tena.

Post a Comment

0 Comments