habari Mpya


Taswira ya Sakata la Maafisa Idara ya Uhamiaji na Wakazi wa Kata ya Kabanga,wilayani Ngara mkoani Kagera.

Ofisi ya Kata ya Kabanga,Ngara,Kagera.

Pichani ni baadhi ya Wakazi wa kata ya kabanga wilaya ya Ngara mkoani Kagera wakati wakiwalalamikia maafisa uhamaji waliokiuka taratibu za utumishi baada ya kuingia kwenye nyumba za raia kwa lazima huku wengine wakiruka kuta za nyumba na kupora mali ambayo thamani haijajulikana. 

 Malalamiko hayo yametolewa May 8, 2018  katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika ofisi ya kata ya Kabanga baada ya waliofanyiwa vitendo vya unyanyaswaji kuhojiwa na watendaji wa uhamiaji ngazi ya mkoa na taifa. 

Picha na Shaaban Ndyamukama -Radio Kwizera Ngara.

Kufuatia Sakata hilo, Kamishna wa huduma kwa mteja na sheria wa idara ya uhamiaji makao makuu nchini Anolile Manyaga aliwaomba radhi wananchi katika mkutano wa hadhara baada ya kufanyika kikao cha ndani kusikiliza malalamiko ya walio fanyiwa vitendo vya udhalilishaji na kuonewa. 

Manyaga alisema hatua za kinidhamu zitachukuliwa kwa maafisa hao kwani wamechafua idara lakini wananchi waendelee kutoa ushirikiano katika kuwaondoa wahamiaji haramu nchini na kwamba taratibu za utumishi zitatumika kuwawajibisha watakaobainika kujihusisha na vitendo hivyo.

 Maafisa uhamiaji  watano wanaotuhumiwa kufanya uhalifu katika mji wa Kabanga wamefikishwa mahakama ya wilaya wakituhumiwa kutenda kosa la jinai kwa kuvunja kifungu cha sheria namba 241 sura ya 16 ya mwaka 2002.

 Hata hivyo watuhumiwa walikana shitaka linalowakabili ambapo wamepata dhamana mpaka May 12 mwaka huu. 


Post a Comment

0 Comments