habari


Taswira Picha ya Mabanda ya Kunasia Senene Mjini Muleba mkoani Kagera.

 Ujenzi wa Mmabanda ya kunasia senene  usiku ukiendelea  eneo la Kamanengo katika Mamlaka ya mji mdogo wa Muleba mkoani Kagera  ambao baadhi ya Wanamuleba wamesema wananufaika na Biashara hiyo.

Picha Na Shaaban Ndyamukama -Radio Kwizera Ngara.
Vyuma chakavu licha ya kupigwa marufuku na vyombo vya ulinzi na usalama kwa kusababisha uvunjifu wa amani kutokana na baadhi ya watu kuvihitaji kwa njia isiyo halalai vimetajwa kuwa mkombozi kwa wanaohitaji kujikwamua kiuchumi.

 Hayo yamebainishwa na Vijana wa kitongoji cha Kamanengo wilaya ya Muleba mkoani Kagera waliokuwa wakitumia vipande vya mabati yaliyochakaa kujenga mabanda ya kunasia senene  usiku wakitumia umeme wa Jenerata ambapo wakati wakongea na Mwandishi wetu ,wamesema wananufaika na mabati hayo.
Aidha mabati hayo pia yanawanufaisha mafundi wa kujenga mabanda hayo kwani wanalipwa ujira na kuonesha ustadi wa fani zao katika kutoa huduma kwa jamii.

Mmoja wa wafanya biashara ya senene katika mji wa Muleba  Abdallah Azizi Ibrahimu amesema  faida anayoipata katika kujikwamua kiuchumi ni sh65,000 kwa ndoo ya  senene.

Picha Na Shaaban Ndyamukama -Radio Kwizera Ngara.


 

Post a Comment