habari Mpya


TASAF – Ngara Wapongezwa kwa Kazi Nzuri.

Muonekano wa Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngara mkoani Kagera katika  Picha ya Pamoja na Wawezeshaji wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF III).

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngara Mkoani Kagera Bw.Aidan John Bahama, amewapongeza Watendaji wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF), kwa kazi nzuri ya kuboresha maisha ya kaya Masikini na kwa miradi ya maendeleo.

Mkurugenzi Mtendaji huyo Bw.Bahama, ametoa pongezi hizo May 21, 2018, wakati wa semina ya wakuu wa Idara wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngara, iliyoendeshwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF III).

Amewataka wakuu hao wa idara kuwa wasikivu, watulivu na makini wakati wote wa semina hiyo, ili iwe ya manufaa kwao kama wataalamu, na kwa walengwa wanaotegemea msaaada wa kitaalamu.

Aidha, Afisa Ufuatiliaji-Kukuza Uchumi wa Kaya Masikini wa Mfuko wa Maendeleo ya jamii (TASAF) Bw.Yohanes Nchimbi, amesema kwamba Mfuko wa Maendeleo ya Jamii unalenga kuongeza uwezo wa kuzalisha kipato cha kaya Masikini.

Mfuko huo una mpango wa kuongeza kipato, fursa na uwezo wa kugharimia mahitaji ya kaya za walengwa, kupitia utekelezaji wa uhawishaji fedha na ajira za muda, mpango wa kuweka akiba na kukuza uchumi, kuboresha miundombinu pamoja na kuwajengea uwezo.

 Mafunzo hayo yatadumu kwa siku tano tangu May 21-25, 2018, na kuwashirikisha wakuu wa Idara ya Halmashauri ya Wilaya ya Ngara, Waheshimiwa Madiwani, Wagani pamoja na Walengwa wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF III).

Post a Comment

0 Comments