habari Mpya


Serikali yaipongeza Karagwe kwa Usimamizi mzuri wa Miradi.

Miongoni mwa madarasa yaliyojengwa kwa uadilifu wilayani Karagwe

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mtaa, Bw.Seleman Jafo amepongeza uongozi wa Halmashauri ya Karagwe kwa usimamizi wa ujenzi wa madarasa na miradi ya maendeleo katika wilaya hiyo.

 Amesema kuwa Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe iliyopo Mkoani  Kagera imetekeleza kwa umakini maagizo ya Serikali ya kutumia fedha zilizotolewa kwa umakini katika ujenzi wa vyumba vya madarasa.

"Nimefurahishwa na maendeleo ya ujenzi wa vyumba vya madarasa na ujenzi wa matundu ya vyoo ambao umesimamiwa kwa weledi mkubwa na kukamilika kwa wakati"

Amewapongeza watumishi wa Wilaya hiyo kwa kufanya kazi kwa weledi kwa kufuata sheria na taratibu za utumishi wa umma ili kuweza kutoa huduma bora kwa jamii.

"Watumishi waliopo chini ya Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa kuwatumikia wanachi kwa weledi ili kupunguza changamoto zinazowakabili kwa kufanya kazi kwa bidii"

Post a Comment

0 Comments