habari Mpya


RC Kigoma - Akagua Zoezi la NIDA Manispaa ya Kigoma Ujiji.

Na Adrian Eustace -Kigoma.

Mkuu wa mkoa wa Kigoma Emmanuel Maganga amefanya ziara fupi ya kutembelea baadhi ya vituo vya uandikishaji wa vitambulisho vya uraia NIDA vilivyopo katika Manispaa ya Kigoma Ujiji mkoani Kigoma na kubaini kuwepo kwa changamoto ya uelewe mdogo wa wananchi juu ya faida za vitambulisho vya uraia.

Katika hatua nyingine Mkuu wa Mkoa amewataka wananchi Mkoani Kigoma kuhusianisha masuala ya siasa na zoezi la utoaji wa vitambulisho vya uraia na kwamba serikali haitawavumilia watakaobainika kufanya hivo.
Kwa upande wake Afisa wa NIDA  mkoani Kigoma Bi. Miliamu, amesema ofisi ya NIDA imeandaa utaratibu Mpya utakao tumika kuwasajiri Wananchi wasiokuwa na baadhi ya nyaraka muhimu kikiwemo Cheti cha kuzaliwa jambo litakalosaidia kuondokana na changamoto ya wananchi kuwalalamikia viongozi wao pale wanapolipishwa fedha ya kiapo kwa mawakili na wanasheria wengine wanaofanya kazi za kuthibitisha nyaraka mbalimbali kisheria.

Post a Comment

0 Comments