habari Mpya


Polisi Shinyang'a wakamata Mali zilizoibiwa na Dawa za Kulevya Mjini Kahama.

 
Vitu vilivyoibiwa katika kampuni ya GSM ya Dar es salam Mjini Kahama mkoani Shinyang’a ambapo Jeshi la Polisi wilayani humo limevikama eneo la Nyihogo.

Picha Na Simon Dioniz -Radio Kwizera -Kahama.

 Kamanda wa Polisi Mkoani Shinyang’a Simon Haule na OCCID George Bagyemu wakionyesha Pikipiki inayodaiwa kutumika kusomba vitu vilivyokuwa vinadaiwa kuibiwa kwenye magari ya kampuni ya GSM mjini Kahama.

 Kamanda wa Polisi Mkoani Shinyang’a Simon Haule na OCCID George Bagyemu na Maafisa wengineo wa Polisi wakionyesha mali mbalimbali zinazodaiwa kuibwa Mjini Kahama.
Katika hatua nyingine,Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga linamshikilia Raia wa nchini Ugiriki kwa tuhuma za kukutwa na kilo moja ya dawa za kulevya aina ya Mrungi akiwa anaendelea kuitumia.

Kamanda wa polisi mkoani humo Bw. Simon Haule amemtaja mtumiwa kuwa ni Bw. Mnasri Shock ambaye ni Dereva wa magari ya kampuni ya FAAR TRACKS ya jijini Dar es salaam.

 
Kamanda Haule amesema kuwa mtuhumiwa alikamatwa katika eneo la Nyihogo ambapo dereva huyo alikuwa akielekea nchini Rwanda akiwa anaendesha gari lenye namba za usajili T.105 DKL likiwa na tela lenye namba za usajili T 544 DKY aina ya Lailend Daf.

Kutokana na hali hiyo mtuhumiwa anaendelea kuhojiwa na kwamba baada ya uchunguzi kukamilika atafikishwa mahakamani kwa kosa la kukutwa na dawa za kulevya na kutumia kinyume cha sharia.

Post a Comment

0 Comments