habari Mpya


Picha- Ujenzi wa Kituo cha Afya Kimeya wilayani Muleba Ulipofikia Sasa.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Muleba mkoani Kagera,Ndg. Emmanuel Sherembi ametembelea na kukagua shughuli za ujenzi na upanuzi wa Kituo cha Afya Kimeya ili kuona maendeleo ya ujenzi huo unaotakiwa kukamilika ifikapo tarehe 31/05/2018. 

Akikagua ujenzi huo hivi karibuni, Ndg. Emmanuel Sherembi amewasisitiza mafundi waliopewa kazi za ujenzi kukamilisha kazi zilizobaki kwa wakati na kuwataka wafanye kazi mchana na usiku ili kuhakikisha wanakamilisha ujenzi ndani ya muda waliopewa.
Kituo cha Afya Kimeya ni miongoni mwa vituo 139 vya awamu ya pili ambavyo kila kimoja kilipewa kiasi cha Tsh. 400,000,000 kutoka Serikali Kuu kwa ufadhili wa World Bank kwa ajili ya upanuzi wa vituo hivyo na hadi sasa Chumba cha Upasuaji, Wodi ya Akina Mama, Nyumba ya Mtumishi, Maabara na Chumba cha kuhifadhia maiti (mortuary) vipo katika hatua ya umaliziaji.

Nyumba ya Mtumishi inayojengwa katika kituo wa Kituo cha Afya Kimeya wilayani Muleba mkoani Kagera.
Jengo la Kuhifadhia Maiti.

Aidha, ujenzi huu umetekelezwa na mafundi wanaopatikana katika maeneo ya wananchi (Local) na kila jengo linafundi anayejitegemea ili kusaidia kukamilisha ujenzi kwa muda uliotolewa.

 Ujenzi huu unasimamiwa na Kamati ya Ujenzi iliyotokana na Bodi ya Kituo cha Afya kwa kushirikiana na wataalamu kutoka ofisi ya Mkurugenzi ambao ni Mhandisi wa Ujenzi, Afisa Manunuzi, Mganga Mkuu na Afisa Mipango. 

Ujenzi huu ulianza mwezi February,2018 na unatarajia kukamilika tarehe 31/05/2018.
Ujenzi wa Wodi ya Akina Mama katika Kituo cha Afya Kimeya
Jengo la Upasuaji katika Kituo cha Afya Kimeya na ujenzi huo unaotakiwa kukamilika ifikapo tarehe 31/05/2018.

Post a Comment

0 Comments