habari Mpya


Picha - Ajali ya Lori yaua Wawili Karagwe.

Na-Elen Magambo -Radio Kwizera,KARAGWE.

Watu wawili wamefariki papo hapo na watatu kujeruhiwa katika ajali ya Lori semi trela aina ya Scania yenye namba za usajili T 720 BJQ kufeli mfumo wa breki na kutumbukia kwenye mtalo eneo la mlima Kishoju wilayani Karagwe mkoani Kagera. 

Mkuu wa wilaya ya Karagwe Godfrey Mheruka amesema ajali hiyo imetokea leo May 29, 2018 majira ya saa Sita mchana wakati Lori hilo lilipotaka kukata kona na kisha kupoteza mwelekeo na kusababisha ajali likiwa na tani 30 za mahindi. 

Godfery Mheluka amewashukuru Wananchi wote waliojitokeza kwa ajili ya kuokoa majeruhi kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi.
 
 
Mkuu wa Upelelezi wilaya Karagwe Anyelwisye Mwakasungula kwa niaba ya Mkuu wa Jeshi la Polisi wilayani humo amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo.

Naye Mganga wa zamu wa hospitali teule ya Wilaya ya Karagwe Nyakahanga Eliusi Bahindi amesema kuwa amepokea majeruhi wawili wakiwa na majeraha sehemu mbalimbali ya miili yao na wanaendelea vizuri.
 
 
 

Post a Comment

0 Comments