habari Mpya


Benki ya NMB Kibondo yasaidia Vitanda na Mashuka Hospitali ya Wilaya.

Hospitali ya Wilaya ya Kibondo Mkoani Kigoma imepokea vitanda na mashuka vyenye thamani ya shilingi milioni 5 vilivyotolewa na Benki ya NMB Tawi la Kibondo katika kuunga mkono utoaji huduma bora ya afya kwa wananchi.

Meneja Kanda ya Magharibi wa Benki hiyo Bw Leoni Ngowi akizungumza katika makabidhiano hayo amesema kuwa msaada huo ni sehemu ya kile ambacho kinachangiwa na Wananchi wa wilaya ya Kibondo kupitia Benki hiyo.

Bw Ngowi amesema wanatarajia msaada huo utapunguza baadhi ya changamoto hususani za wagonjwa kukosa sehemu za kupumzika wakati wakipatiwa huduma.
Awali akizungumzia hali ya uhaba wa vitendea kazi katika Hospitali ya wilaya hiyo, Mganga mkuu wa wilaya ya Kibondo, Dr Pima Sebastian amesema vitu hivyo vitasaidia wao kutoa huduma kwa ufasaha ikiwa ni pamoja na kupunguza swala la wagonjwa wawili kutumia kitanda kimoja.

Na- Faraja Marco –Radio Kwizera KIBONDO.

Post a Comment

0 Comments