habari Mpya


Muleba yanunua Boti ya Doria za Uvuvi ili kuimarisha Ulinzi na Usalama Ziwani.

Halmashauri ya wilaya ya Muleba mkoani Kagera imenunua Fiber Patrol Boat –Horse Power 40 yenye Thamani ya Shilingi milioni 53.1 fedha iliyotokana na makusanyo ya mapato ya ndani kwa mwaka 2016/2017.

 
Boti hiyo inauwezao wa kubeba abiria 12 na tani moja ambapo itakuwa mahususi kwa ajiri ya kufanya doria  za uvuvi katika mipaka ya ziwa victoria wilayani Muleba.
 
Boti hiyo ikiwa tayari imeshushwa Ziwani.

 
Boti hiyo imepokelewa leo May 25, 2018 katika mwalo wa Katembe na kufanyiwa majaribio kuelekea katika mwalo wa Kyamkwikwi wilayani humo.

Picha Na Shafiru Yusuf –Radio Kwizera Muleba.
 
 

Post a Comment

0 Comments