habari Mpya


Muleba -Daraja lakatika na Wanafunzi Kushindwa Kuvuka.

Baadhi ya Wanafunzi wa Shule ya msingi Bugara iliyopo Kata ya Rulanda wilayani Muleba  mkoani Kagera wameshindwa kuhudhuria masomo yao shuleni hapo baada  ya  daraja liliokuwepo la muda kusombwa na maji.

Habari/Picha Na Shafiru Yusufu –Radio Kwizera MULEBA.

Mwalimu mkuu wa shule hiyo Bw. Rwezahura Renard amesema kuwa mvua hiyo imeanza  kunyesha majira ya usiku wa kuamkia leo May 15, 2018 hivyo wameomba Mamlaka husika kuwatengenezea daraja hilo Ili kurejesha mawasiliano na Wanafunzi waendelee kupata masomo yao.
Kwa upande wake Diwani  wa Kata hiyo Bw. Evart Ernest amesema kuwa amelitolea taarifa kwa Mamlaka husika hivyo mpaka sasa bado utekelezaji wake na kwamba jitihada za haraka zinahitajika ili kuepusha madhara yanayoweza kujitokeza kwa Wanafunzi wanaotukia kivuko hicho.

Post a Comment

0 Comments