habari Mpya


Mkwamo huu wa Lori Eneo la Kijii cha Nyabibuye wilaya ya Kakonko mkoani Kigoma.

Vijana wa kijii cha Nyabibuye wilaya ya Kakonko mkoani Kigoma wakihamisha magunia ya Tangawizi kutoka kwenye  Lori ambalo lilishindwa kupita kwenye daraja la kijiji hicho hivi karibuni kutokana na wingi wa magunia na barabara kudidimia  ikiwa kwenye matengenezo . 
Magunia ya Tangawizi yalikuwa yakisafirishwa kutoka  wilaya ya Kasulu mkoani humo hadi mkoa wa Muyinga nchini Burundi.

 Aidha barabara nyingine iliyo na usumbufu ni ile ya kutoka Mukalunzi kwenda Murusagama  wilayani Ngara ambako daraja limerundwa na mawe na magari yanayopita ni yenye tani moja lakini malori ya mizigo yakipita kuna hatari ya kutotoka ikiwa ni pamoja na barabara ya kutoka Murusagamba kuelekea daraja linalotenganisha wilaya ya Ngara na Kakonko.


Na- Shaaban Ndyamukama -Radio Kwizera.
Katika daraja hilo Wafanyakazi wa Radio Kwizera  hivi karibuni  walilazimika kusubiria kusombwa kwa magunia  hayo ya tangawizi wapate njia ya kupita wakati wakitokea wilaya ya Kibondo  mkoani kigoma kwenye zoezi la uhamasishaji kuchangia damu wakielekea wilayani Ngara mkoani Kagera.

Post a Comment

0 Comments