habari Mpya


Mkoa wa Kigoma na Mapambano dhidi ya Virusi vya Ebola.

Mtalamu akionesha namna ya kuvaa Mavazi maalumu ya kujikinga na Ebola kwa Wadau wa Afya mkoani Kigoma May 16,2018.
  
Mganga mkuu wa Mkoa wa Kigoma Dkt.Paul Chaote amesema Serikali ya mkoa huo kupitia idara ya afya imechukua hatua za awali katika kukabiliana na maambukizi ya Ugonjwa wa Ebola ulioripotiwa nchi jirani ya Kongo
Dkt.Chaote amesema hayo katika kikao cha wadau wa afya ngazi ya mkoa kilichofanyika kwa lengo la kudhibiti uwezekano wa kuenea kwa maambukizi ya ugonjwa huo.

Aidha amesema kwa upande wa Halmashauri za wilaya ya Kibondo na Kakonko wametenga vituo hivyo katika vituo vya afya Mabamba na Gwanumpu, Hospitali ya wilaya ya Kibondo pamoja na kambi za Wakimbizi za Nduta na Mtendeli.
Kwa upande wake Mkuu wa mkoa wa Kigoma Brigedia Generali Mstaafu Emmanuel Maganga amewataka wataalamu wa afya mkoani humo  kuhakikisha wanafanya kazi zao  kwa weledi ikiwa ni pamoja na kutoa elimu kwa Wananchi  juu ya dalili za awali za ugonjwa huo.

Nchi ya DRC imekuwa na milipuko mingi  ya Ebola kuliko nchi yoyote duniani. Katika kipindi cha miaka 10 iliyopita kumekuwa na milipuko 5 ambayo ni mwaka 2007, 2008 hadi 2009, 2012, 2014 na 2017.

Kwa taarifa zilizopo, tayari watu 23 wamefariki kutokana na ugonjwa wa virusi vya Ebola nchini Congo DRC.

Ebola ni ugonjwa unaotokea katika kipindi fulani na kuua watu wengi kwa muda mfupi.

Habari Na Adrian Eustaus Radio Kwizera KIGOMA.

Post a Comment

0 Comments