habari Mpya


Miradi 14,051 ya Kunusuru Kaya Maskini wilayani Ngara yatumia Bilioni 502.

Akina Mama wa Buhororo,Ngara wakisikiliza kwa makini maelezo juu ya Mradi.

 Jumla ya miradi elfu 1na 704 yenye thamani ya shilingi bilioni 72 imetekelezwa na mpango wa kunusuru kaya maskini TASAF awamu ya kwanza na miradi elfu 12 na 347 yenye thamani ya shilingi bilioni 430 imetekelezwa katika awamu ya pili.

 
Mkuu wa wilaya ya Ngara.

Taarifa hiyo imetolewa na mkuu wa wilaya ya Ngara Luteni Kanali Michael Mtenjele wakati akifungua mafunzo ya TASAF kwa wakuu wa idara mbalimbali katika ukumbi wa halimashauli wilayani humo.

Aidha mratibu wa TASAF kutoka makao makuu taifa Bw Yohana Issa Nchimbi amesema mafunzo hayo pia yatashirikisha madiwani na maafisa ugani ambao mara nyingi wanapata changamoto za walengwa walioko kaya maskini.

Mafunzo hayo yana lengo la kuwapa wakuu wa idara mbizu za utambuzi wa uwekaji akiba na kukuza uchumi wa kaya zinazonufaika na mpango wa kunusuru kaya maskini TASAF wilayani Ngara

Post a Comment

0 Comments