habari Mpya


Miongoni mwa Habari zilizosikika Saa 24 zilizopita Radio Kwizera FM.

Source; RK, kj (Maagizo)
Ed: AG
Date: Monday, May 07, 2018

KYERWA

Afisa elimu shule za sekondari wilayani Kyerwa mkoani Kagera Bw. Fracins Inshainja amewataka wazazi na walezi wilayani humo kujenga tabia ya kuwachangia watoto wao chakula ili kuwasaidia kukua kitaluma wawapo shuleni

Bw. Inshainja ametoa kauli hiyo kwenye sherehe za kuapisha wanafunzi elfu 1 na 353 wa skauti wa shule za msing na sekondari zilizofanyika katika shule ya msingi Karo

Mkuu wa Wilaya Kyerwa Kanal Shaban Lissu amewataka skauti hao kuendelea kuongeza mafunzo ili kuwa mashunjaa katika kuilinda nchi yao kikamilifu na kujenga tabia ya kuisaidia jamii pale matatizo yanapojitokeza

Nao baadhi ya wazazi waliohudhuria sherehe hizo wameahidi kuchangia chakula kwa watoto wao na kushirikiana katika kuwapa malezi bora yatakayoweza kuwasaidia katika jamii inayowazunguka 


Source; RK, Elias z (unyanyasaji)
Ed: AG
Date: Monday, May 07, 2018

CHATO

Mwanafunzi Felista John anayesoma darasa la saba katika shule ya msingi Chato iliyopo wilayani Chato mkoani Geita ameiomba Serikali kumsaidia dhidi ya ukatili anaotendewa na baba yake pamoja na mama yake wa kambo ili kuhakikisha anatimiza ndoto zake za kielimu

Akihojiwa na radio kwizera mtoto huyo ameeleza kuwa amekuwa akikumbana na kipigo cha mara kwa mara, kunyimwa Chakula pamoja na kulazimishwa aombe ruhusa shuleni kwa kisingizio cha ugonjwa ili arudi kucheza na mtoto wa mama kambo nyumbani

Insert............Felista John
Cue In……….
Cue Out………..

Baba mzazi wa mtoto huyo Bw. John Abel amesema kuwa mwanae haelewani na mama yake wa kambo na kwamba adhabu ya kunyimwa chakula ni mbadala kwakwe kwani huitoa kwa watoto wote wanapokuwa wamekosea

Afisa ustawi wa jamii wilayani Chato Bw. Onesmo Ntoze amesikitishwa na kitendo hicho ambapo ameahidi kuchukua hatua za kisheria kwa wahusika baada ya kukamilisha uchunguzi wake ikiwa ni pamoja na kumhakikishia mtoto mazingira salama

Insert..........Onesmo Ntoze
Cue In……….
Cue Out………..

Aidha Bw. Ntoze ameaomba jamii kushirikiana katika kutoa taarifa kwa vyombo husika juu ya vitendo vya ukatili na unyanyasaji vinavyolenga kukandamiza haki za binadamu


Source; RK, wm (kujinyonga)
Ed: AG
Date: Monday, May 07, 2018

MISSENYI

Mwanaume Felesian Festo mwenye umri wa miaka 67 mkazi wa kitongoji cha Nyabishere kata ya Kyaka wilayani Missenyi Mkoani Kagera amekutwa amejinyonga kwa kutumia kamba iliyokuwa inatumika kufungia mbuzi

Mwenyekiti wa kijiji cha Kashaba ambacho kuna kitongoji cha Nyabishere Bw. Domician Kaijage amesema tukio hilo limetokea Mei 5 mwaka huu majira ya saa tatu asubuhi

Amesema baada ya uongozi wa kijiji kufika eneo la tukio, umelitaarifu jeshi la polisi ambalo baada ya kufika na kufanya uchunguzi limeruhusu familia kuuchukua mwili na kuendelea na taratibu za mazishi

Kwa upande wake mkuu wa jeshi la polisi wilayani Missenyi Bw. Tomas Kiondo amesema bado hawajabaini chanzo cha tukio hilo linaendelea na uchunguzi


Source; RK, p.g (mgomo wa walimu)
Ed: AG
Date: Monday, May 07, 2018

KASULU

Walimu waliohamishwa kutoka shule za sekondari kwenda masingi katika halmashauri ya mji wa Kasulu mkoani Kigoma, wameazimia kuendesha mgomo Baridi na kutofika kwenye vituo vyao walivyopangiwa, mpaka watakapopewa stahiki zao zote

Maamuzi hayo yamefikiwa hii leo wakiwa nje ya ofisi ya mkurugenzi wa halmashauri ya mji wa Kasulu Bi. Fatina Laayi wakidai kupata mwafaka juu ya malipo yao ya uhamisho ili waweze kuwajibika katika shule walizopangiwa

Walimu hao wameiambia Radio Kwizera kuwa wamefuatilia zaidi ya miezi mitatu sasa tangu kutolewa kwa agizo hilo lakini mpaka sasa hawajapatiwa stahiki zao huku nao wakiahidi kutofika katika vituo walivyopangiwa mpaka stahiki zao zitakapolipwa

Insert……….Walimu
Cue in…………..
Cue out……….

Katibu wa Chama cha walimu (CWT) wilayani Kasulu Mwl. Buchumi Felister Nkayamba, amesema msimamo wa chama cha walimu ni kuitaka halmashauri hiyo kuwalipa walimu stahiki zao kama maelekezo ya Raisi yanavyoelekeza

Hata hivyo mkurugenzi wa halmashauri ya mji wa Kasulu Bi. Fatina Laayi, alipoulizwa kuhusu malalamiko ya walimu hao amesema hayupo tayari kulizungumzia suala hilo ambapo radio kwizera inaendelea kufuatilia kwa ajili ya kupata majibu 


Source; RK, Ak (mauaji)
Ed: AG
Date: Monday, May 07, 2018

BUKOBA

Jeshi la polisi mkoani Kagera linamshikilia Bw. Rweyemamu Emmanuel wa miaka 27 mkazi wa kijiji cha Kyota Tarafa ya Kimwani wilayani Muleba kwa tuhuma za kumuua mke wake Sikujua Paschal

Akizungumza na wanahabari, Kamanda wa jeshi la polisi mkoani Kagera Agustino Ollomi amesema mauaji hayo yametokea kufuatia kuwepo kwa ugomvi baina ya wanandoa hao uliosababishwa na wivu wa kimapenzi ambapo mwanamke alikuwa kimtuhumu mume wake kutoka nje ya ndoa

Amesema kuwa jeshi la polisi pia linamtafuta mwanamke anayetajwa kuwa kisababishi cha ugomvi huo anayefahamika kwa jina moja la Tedi ambaye alikimbia baada ya tukio ili alisaidie jeshi hilo katika shughuli za upelelezi

Insert………..Kamanda Ollomi
Cue in……….
Cue uou……..

Katika tukio lingine Kamanda Ollomi amesema moto ambao haujafahamika chanzo chake umeteketeza nyumba mali ya Yusuph Hassan mkazi wa kata Miembeni katika manispaa ya Bukoba na kusababisha hasara ya mali zilizokuwemo

Tukio hilo limetokea jana majira ya saa 1 jioni na kwamba samani na vitu vilivyokuwemo kwenye nyumba hiyo bado havijajulikana thamani yake na uchunguzi wa kipolisi unaendelea ili kujua chanzo cha moto huo 

Baadhi ya wakazi wa manispaa ya Bukoba wamesema kuwa matukio ya watu kujichukulia sheria mkononi yanaendelea kuwepo kutokana na watu kutokuheshimu sheria zilizowekwa


Source; RK: SR. OLIVER (Madhara ya mvua)
Ed: AG
Date: Monday, May 07, 2018

NGARA

Mvua zinazoendelea kunyesha katika wilaya ya Ngara mkoani Kagera zimekata mawasiliano baina ya kata ya Mbuba na Bukiriro baada ya daraja la Mukajagali linalounganisha kata hizo kujaa maji na wananchi kukosa sehemu ya kupita kutafuta huduma za kijamii

Wakizungumzia tatizo hilo, wakazi wa kijiji cha Kumwendo kata ya Mbuba wamesema, wanavuka kwa mitumbwi isiyokuwa na viwango kiusalama huku wakihofia maisha yao

Kwa mujibu wa mwenyekiti wa kijiji cha Kumwendo Bw. Bruno Frednandi, daraja hilo linahitaji kuinuliwa na kupanuliwa ili kusaidia wananchi wanaokwenda kutafuta huduma za matibabu na watoto wadogo wanaohitaji kuvuka kwenda shule ya msingi Kumwendo.

Insert……… Bruno Kumwendo
Cue in………….
Cue out………….

Meneja wa TARULA wilayani Ngara Bw. Subira Manyama amekiri kuifahamu changamoto hiyo na kusema kuwa upo mpango wa kujenga daraja hilo la mkajagali hivyo wananchi wawe na subira

Insert……….Subira Tarula
Cue In…….
Cue out…….

Post a Comment

0 Comments