habari Mpya


Mganga Mfawidhi Kakonko Ajinyonga na Taulo Ndani ya Chumba Chake.

Mwili  wa Dkt. Mejo Banikira  ukiondolewa nyumbani alikojinyongea  kwa kutumia gari la Wagonjwa na kwenda kuhifadhiwa Hospitali ya Kibondo wakati Jeshi la Polisi likiendelea na uchunguzi.

 Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya Kakonko, mkoani Kigoma , Dkt. Mejo   Banikira (43) amekutwa amejinyonga chumbani kwake kwa kutumia taulo yake.

Mkuu wa Wilaya ya Kakonko, Kanali Hosea Ndagala akitoa taarifa ya tukio hilo leo May 29,2018  amesema   uchunguzi unaendelea ili kubaini chanzo cha daktari huyo kujiua.

Picha Na Faraja Marco –Radio Kwizera Kakonko.
Baadhi ya Viongozi na Wananchi wakiwa na nyuso za huzuni kufuatia tukio hilo ambapo kwa Mujibu wa Mashuhuda wamebainisha kuwa Marehemu alikuwa akiishi peke yake katika nyumba za kupanga mjini Kakonko.
Post a Comment

0 Comments