habari


Mbunge BILAGO -‘Ugomvi’ wa Serikali na Shule Binafsi, ni Wivu tu.

Seerikali imetakiwa kuzihudumia vyema shule zake na kuboresha mazingira na miondombinu ya kufundishia ili ziweze kushindana na shule binafsi ambazo zimekuwa zikifanya vizuri katika mitihani hususan shule za msingi na sekondari.

Hayo yamesemwa na Mbunge wa Kakonko mkoani Kigoma, Kasuku Bilago, wakati akichangia hoja katika mjadala wa bajeti ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia iliyowasilishwa Bungeni jijini Dodoma ambapo amesma shule za serikali zimekuwa zikifanya vibaya katika mitihani hiyo, jambo ambalo litaendelea kudidimiza elimu nchini.

Akiendelea kuchangia bajeti hiyo iliyowasilishwa na Waziri, Profesa. Joyce Ndalichako, Bilago alisema kwenye shule za binafsi kuna motisha kwa walimu na mpangilio mzuri wa ufundishaji, jambo ambalo linafanya shule hizo kufaulisha zaidi ikilinganishwa na shule za serikali ambazo walimu wake wanadai malimbikizo ya malipo yao, hawana nyumba za kuishi, morali ya kufundisha imeshuka na mazingira magumu ya kufundishia ikiwemo vitabu, maabara na vifaa vingine vya nadharia na vitendo.

Aidha, Bilago amedai ‘ugomvi’ kati ya serikali na shule  binafsi ni wivu tu wa serikali kutotaka kushindwa huku akiwataka kuiga mfano na mifumo inayotumiwa kwenye shule hizo binafsi ili kuinua ufaulu wa wanafunzi.


Post a Comment