habari Mpya


Kumuyange FC (Kagera) yapata ushindi wa pili mfululizo wa Ligi ya Mabingwa wa Mikoa.

Wachezaji wa Kumuyange FC wakishangilia moja ya goli walilolifunga leo May 11,2018 dhidi ya Ambassador FC ya Simiyu baada ya kukubali kufungwa bao 3-2 katika mchezo makali na wakusisimua kwenye uwanja wa WAJA mjini Geita licha ya kuhudhuriwa na Mashabiki wachache.
Kikosi cha Kumuyange FC ya Kagera.

Kumuyange FC (Kagera) wamepata ushindi wa pili mfululizo wa Ligi ya Mabingwa wa Mikoa (RCL 2017/2018). 
Kikosi cha Ambassador FC ya Simiyu.
Kwa maana hiyo, pointi 6 ambazo wamejikusanyia Kumuyange FC hadi sasa zinawafanya waongoze Kundi lao la A la michuano hiyo,wakifuatiwa na Ungindoni FC ( DSM) wenye point  4,Phantom FC (Mwanza) point 4 na Gipco FC (Geita) wenye Point 2.

Hapa Chini ni Matokeo ya Mechi zote za Jana May 10, 2018.

Post a Comment

0 Comments