habari Mpya


Kanali Hosea Ndagalla –‘’Kakonko Saccos iwe Chachu ya Vijana Kujiunga na Vyama vya Ushirika’’.

Mkuu wa wilaya ya Kakonko mkoani Kigoma Kanali Hosea Ndagalla akiongea na Vijana wakati wa ufunguzi wa Chama cha USHIRIKA CHA KAKONKO SACCOS  baada ya chama hicho kusambaratika kwa miaka kadhaa kutokana na kukosa msimamo kutoka kwa Viongozi.

Habari/Picha Na-Faraja Marco -Radio Kwizera Kakonko.

 Kanali Hosea Ndagalla amewataka Vijana wilayani humo kujiunga na vyama vya ushirika ili kujikwamua kiuchumi badala ya kutumia muda mwingi katika maeneo ya starehe.

Kanali Ndagalla amesema ni jambo la kushangaza kuona vijana wengi wakitumia muda mwingi katika maeneo ya starehe wakati kuna fursa zinazoweza kuwainua katika masiha yao.

Kwa upande wake Afisa Ushirika wilayani Kakonko Bw. Braison Mkalawa amesema Serikali imeamua kutilia maanani katika kufufua Vikundi vya Ushirika hivyo ni Vyema wanaojiunga kuhakikisha wanajisimamia ipasavyo.


Post a Comment

0 Comments