habari Mpya


Job Ndugai - Tanzania inautambua Mchango wa Vyombo vya Habari.

GROUP%2B2
 Mgeni rasmi Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Job Ndugai katika picha ya pamoja na baadhi ya wadau wa habari na wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa, Ubalozi wa Umoja wa Ulaya pamoja na wamiliki wa vyombo vya habari vya kijamii waliohudhuria kongamano la maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari nchini yanayofanyika katika Hoteli ya Morena jijini Dodoma
GROUP%2B3
 Mgeni rasmi Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Job Ndugai katika picha ya pamoja waandishi wa habari wakonge (Veterans) waliohudhuria kongamano la maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari nchini yanayofanyika katika Hoteli ya Morena jijini Dodoma.
GROUP%2B4
 Mgeni rasmi Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Job Ndugai katika picha ya pamoja mameneja wa redio za kijamii waliohudhuria kongamano la maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari nchini yanayofanyika katika Hoteli ya Morena jijini Dodoma.
GROUP%2B5
Mgeni rasmi Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Job Ndugai katika picha ya pamoja wanafunzi wa Dodoma College of Journalism waliohudhuria kongamano la maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari nchini yanayofanyika katika Hoteli ya Morena jijini Dodoma.

MC
 Mshehereshaji wa sherehe za maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari, Innocent Mungy akiwakaribishwa meza kuu, wanahabari na wadau wa habari kwenye kongamano la  maadhimisho hayo yanayofanyika katika Hoteli ya Morena jijini Dodoma.
MEZA
 Meza kuu kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA-TAN), Salome Kitomari, Mgeni rasmi Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Job Ndugai, Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkazi wa Unesco ambaye pia ni Mshauri wa Masuala ya Mawasiliano Kanda ya Afrika Mashariki ofisi ya Unesco Nairobi, Jaco Du Toit pamoja na Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Vilabu vya Waandishi wa Habari nchini (UTPC), Jane Mihanji.
NDUGAI%2BSPEECH
 Mgeni rasmi Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Job Ndugai akifungua kongamano la maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari yanayofanyika katika Hoteli ya Morena jijini Dodoma.
JACO%2BSPEECH
 Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkazi wa Unesco ambaye pia ni Mshauri wa Masuala ya Mawasiliano Kanda ya Afrika Mashariki ofisi ya Unesco Nairobi, Jaco Du Toit akitoa salamu za Unesco wakati wa kongamano la maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari yanayofanyika katika Hoteli ya Morena jijini Dodoma.
MIHANJI
 Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Vilabu vya Waandishi wa Habari nchini (UTPC), Jane Mihanji akizungumza kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Job Ndugai kufungua kongamano la maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari yanayofanyika katika Hoteli ya Morena jijini Dodoma.
STELLA%2BSDGs
 Afisa Habari wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Stella Vuzo akizungumzia malengo ya maendeleo endelevu na jukumu la waandishi wa habari kutumia nafasi zao kutoa taarifa kuhusu malengo hayo kwa jamii ili yatekelezeke kwa urahisi, katika kongamano la maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari nchini yanayofanyika katika Hoteli ya Morena jijini Dodoma.
ROSE%2BHAJI
 Mtaalamu wa Masuala ya Vyombo vya Habari na Mkufunzi wa kujitegemea, Rose Haji Mwalimu akiongoza mjadala kuhusu mada: Wajibu wa Uongozi, Vyombo vya Habari na Sheria katika kuhakikisha haki inatendeka na kuonekana inatendeka wakati wa kongamano la maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari nchini yanayofanyika katika Hoteli ya Morena jijini Dodoma.
NDIMARA
Mwandishi wa Habari Nguli, Ndimara Tegambwage na mwezeshaji wa mada inayohusu; Wajibu wa Uongozi, Vyombo vya Habari na Sheria katika kuhakikisha haki inatendeka na kuonekana inatendeka: wakati wa kongamano la maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari nchini yanayofanyika katika Hoteli ya Morena jijini Dodoma.
JAMES
Wakili na Mwandishi wa Habari ambaye pia ni Mjumbe wa Bodi ya MISA-TAN, James Marenga akichangia mada wakati wa kongamano la maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari nchini yanayofanyika katika Hoteli ya Nashera jijini Dodoma.
SUNGURA
 Mdau wa Habari Ernest Sungura akishiriki kuchangia maoni katika mjadala uliowasilishwa na mwandishi nguli Ndimara Tegambwage (hayupo pichani) wakati wa kongamano la maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari nchini yanayofanyika katika Hoteli ya Morena jijini Dodoma.
NANCY
Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano na Habari Unesco nchini, Nancy Kaizilege (kulia) na Mshauri wa Utawala Bora na Haki za Binadamu wa Ubalozi wa Sweden nchini, Anette Widholm Bolme wakati wa kongamano la maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari nchini yanayofanyika katika Hoteli ya Morena jijini Dodoma.
WASHIRIKI%2B2
WASHIRIKI%2B3
WASHIRIKI%2B4

WASHIRIKI%2B5
WASHIRIKI%2B7
Pichani juu na chini Sehemu ya washiriki ambao ni wahariri, waandishi wa habari, wadau wa tasnia ya habari na wageni waalikwa waliohudhuria kongamano la maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari nchini yanayofanyika katika Hoteli ya Morena jijini Dodoma.

Na Mwandishi wetu, Dodoma

Waandishi wa habari wanapaswa kuandika na kutangaza habari zao kwa weledi na kuzingatia maadili ili kuepuka kuandika habari zinazoipa serikali sababu ya kufungia vyombo vyao.

Kauli hiyo imetolewa mwandishi wa habari mkongwe nchini Tanzania Bw. Ndimara Tegambwage wakati akitoa mada ya uhuru wa vyombo vya habari nchini Tanzania kwenye kongamano la maadhimisho ya siku ya Uhuru Wa Vyombo vya Habari Duniani ambayo nchini Tanzania yanafanyika kitaifa mkoani Dodoma.

Kila Mei 2-3 kila mwaka ni siku za kimataifa ya Uhuru wa Vyombo vya Habari duniani.

Aidha katika mada yake hiyo Ndimara alisema Serikali barani Afrika zimekuwa zikikosa uvumilivu na kunyima uhuru vyombo vya habari licha ya kuwa uhuru huo unatambuliwa na katiba za mataifa ya Afrika.

Bw. Ndimara amebainisha kuwa, wakati serikali za Africa zikitoa haki ya kusajili vyombo vya habari hususani Radio, Runinga na Magazeti, serikali zinapokosolewa huvifungia vyombo hivyo kwa tuhuma za kukiuka maadili jambo ambalo alidai kuwa si la ukweli.

Awali akitoa hotuba ya ufunguzi wa kongamano la maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari nchini Tanzania, Spika wa Bunge la Tanzania Job Ndugai amesema Tanzania inautambua mchango wa vyombo vya habari katika kurahisisha mawasiliano ya jamii na kuharakisha maendeleo lakini inakwazwa na kuwepo kwa baadhi ya vyombo vya habari na wanahabari ambao huandika habari nyingi za kutungwa na za uongo.

Katika hotuba hiyo alilaani matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii akitaja kuwa inaongoza kwa kuwa na habari nyingi za kujitungia na zenye upotoshaji na kwamba Bunge ni mhanga wa upotoshaji wa habari zinazoandikwa na baadhi ya waandishi katika mitandao ya kijamii.

Akizungumzia ufanisi wa vyombo vya habari na wanahabari wenyewe Spika Ndugai aliwataka waandishi kuwa marafiki na kuacha tabia za kudharauliana  na kushauri ipo haja ya kuwekana sawa kwa maslahi mapana zaidi ya kitaaluma na jamii kwa ujumla.

Pia alizungumzia vyombo vya habari kusaidia mapambano dhidi ya rushwa na ufisadi na kusema kalamu ikitumika vyema itasaidia sana mapambano hayo.

Naye Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkazi wa Unesco ambaye pia ni Mshauri wa Masuala ya Mawasiliano Kanda ya Afrika Mashariki ofisi ya Unesco Nairobi, Jaco Du Toit amesema vyombo vya habari ni muhimu kwa maendeleo kwa hiyo ni lazima viwe huru ili viweze kutekeleza kazi yake.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA-TAN), Salome Kitomari, alieleza kusikitishwa kwake na matukio yanayoashiria kubinya uhuru wa vyombo vya habari  na pia kuitaka serikali kuwajibika katika kuwalinda waandishi wa habari.

Wawakilishi wa radio jamii Tanzania wanasema pamoja na kufanyakazi kubwa ya kuelimisha jamii vijijini, serikali haijavipatia kipaumbele kama inavyofanya kwa vyombo vikubwa na vya kitaifa.

Akizungumza na waandishi wa habari Kiongozi wa Kituo cha Habari cha mkoani Radio FM cha visiwani Pemba Bw. Maalim Ali Abass alisema Radio za vijijini zinapokumbwa na kosa lolote la kitaaluma mema mengi wanayofanya kwa kujitolea husahaulika haraka na kujikuta katika hekaheka na serikali.

Post a Comment

0 Comments