habari Mpya


Idara ya Elimu Sekondari Ngara yapokea zaidi ya Shilingi Milioni 171 za Elimu Bila Malipo.

Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Rusumo.

 Katika kipindi cha robo ya tatu Idara ya Elimu Sekondari kupitia shule za Sekondari 23, katika Halmashauri ya Wilaya ya Ngara,mkoani Kagera imepokea shilingi milioni 171,139,189.00 kwa ajili ya elimu bila malipo, katika kipindi cha Januari hadi Machi 2018.

Kaimu Afisa Elimu idara ya Elimu sekondari ,Bw. Marton James, amedhihirisha hayo wakati wa kikao cha robo ya tatu, kilichofanyika mwishoni mwa mwezi Aprili 2018, katika ukumbi wa Halmashauri.

Amechanganua kwamba katika kipindi hicho, idara yake imepokea jumla ya shilingi milioni 25,425,297.00, ikiwa ni fedha ya fidia ya ada kwa shule za kutwa, ambapo shilingi  milioni 115,528,416.00, zimetolewa kwa ajili ya kununua chakula kwa wanafunzi wa bweni.

Pia tumepokea shilingi milioni 18,685,476.00, ili zitumike kwa ajili ya uendeshaji, ambapo shilingi milioni 11,500,000.00, tumezipokea na tumelipa wakuu wa shule za sekondari posho ya madaraka.” Alisema Bw. James.

Kaimu huyo wa elimu sekondari Bw.James, ameishukuru serikali kwa kupeleka fedha ya elimu bila malipo kwa wakati, kwa sababu hiyo shule 23 za sekondari wilayani humo, zimefanikiwa kuendesha shule hizo kwa urahisi.

Aidha, ameongeza kwamba idadi ya wanafunzi waliochanguliwa kujiunga na kidato cha kwanza katika mwaka 2018, imeongezeka kutoka 3288 hadi kufikia wanafunzi 3826.

Kaimu huyo wa sekondari hakusita kutanabahisha kwamba, idara yake ina upungufu wa walimu wa sayansi hasa wa hisabati, na  wataalamu wa maabara na kwamba jumla ya maabara 69 hazijakamilika ujenzi wake, kwani ni zimekamilika maabara 22 tu.

Post a Comment

0 Comments