habari Mpya


Halmashauri ya Ngara yatumia Zaidi ya Shilingi Bilioni 23.2 kwa Ajili ya Miradi ya Maendeleo.

Madiwani wa Baraza la Halmashauri ya Wilaya ya Ngara mkoani Kagera.
Halmashauri ya Wilaya ya Ngara mkoani Kagera hadi kufikia Machi 31, 2018, ilipokea shilingi bilioni 23,343,040,898.46, na kutumia shilingi bilioni 23,286,911,246.00/=, kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo robo ya tatu 2017/2018.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngara, Bw.Aidan John Bahama, amesema hayo wakati wa Baraza la Madiwani Mei 15, 2018, lililofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya wilaya hiyo.

Bw. Bahama amefafanua kuwa katika kipindi cha Mwaka wa fedha 2017/2018, Halmashauri yake iliidhinishiwa na Serikali kuu Jumla ya shilingi bilioni 44,055,604,713.00; ambapo shilingi  bilioni 28,615,809.00 zilitengwa kwa ajili ya kulipa mishahara ya watumishi.

“Tulitengewa kiasi cha shilingi bilioni 1,165,473,000.00 kwa ajili ya matumizi mengineyo, shilingi milioni 178,248,044.00 ziliidhinishwa kama mapato yatakayotokana na vyanzo vya Halmashauri, ambapo shilingi bilioni 12,492,185,457.00, ilitengwa kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo kutoka Serikali kuu.” Alisema Mkurugenzi Mtendaji.

Tangu July, 2017 hadi March 31, 2018 Halmashauri ilipokea Jumla ya shilingi bilioni 23,343,040,898.46, ambapo mchanganuo wa fedha iliyopokelewa ameutaja kuwa shilingi milioni 912,158,832.05, ilikusanywa kutoka katika vyanzo vya Halmashauri.

Jumla ya shilingi bilioni 17,087,159,760/= ilipokeliwa kutoka Serikali kuu, kwa ajili ya kulipa mishahara ya watumishi, ambapo kiasi cha shilingi milioni 703,720,000/= kilipokelewa toka Seririkali kuu, kwa ajili ya matumizi mengineyo, pamoja na shilingi bilioni 4,640,002,306.45, kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

Aidha, Halmashauri ya Wilaya ya Ngara  imetumia zaidi ya shilingi bilioni 23.2 kwajili ya kulipa mishahara ya watumishi, kutekeleza miradi ya maendeleo katika Sekta za Afya, Elimu na Maji, pamoja na Matumizi mengineyo.


Bw.Bahama amesema kwamba Halmashauri yake imefikia wastani wa 35% ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika sekta mbalimbali, na kwamba tangu July, 2017 hadi march 31, 2018 Halmashauri yake, imetumia zaidi ya shilingi bilioni 4.6; fedha za Mfuko wa Maedeleo ya Jamii (TASAF III), HSBF, Mfuko wa Jimbo, ICAP/MHD na Mfuko wa Maji, kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo.

Post a Comment

0 Comments