habari Mpya


Halmashauri ya Ngara yapokea Zaidi ya Shilingi Milioni 985.4 Kutoka TASAF.

Halmashauri ya Wilaya ya Ngara katika kipindi cha Januari hadi Machi 2018, imepokea kiasi cha shilingi 985,438,660.00 toka Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF), kwa ajili ya kutekeleza mpango wa kunusuru kaya masikini (TASAF III).
Mratibu wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) Bw. Sakina Chamiti, aliyasema hayo Mei 16-17, 2018 wakati wa kikao cha Baraza la waheshimiwa madiwani kilichafanyika katika ukumbi wa Halmashauri.

Tulipokea shilingi 507,224,000.00 ambazo tulizitumia katika kutekeleza uwasilishaji wa fedha, na kiasi cha shilingi 478,214,660 tulizitumia katika mradi wa kutoa ajira za muda (PWP) kwa walengwa wetu.” Alisema Bw.Chamiti.

Amesema katika kipindi cha Januari hadi Februari 2018, Halmashauri ilipokea shilingi 253,796,000.00, ambapo shilingi 253,224,000.00 zimetumika na shilingi 572,000.00 hazijatumika.

Bw.Chamiti amesema katika kipindi cha Machi – Aprili 2018, walipokea shilingi 253,428,000.00, kwa ajili ya kuwalipa walengwa, na kwamba zoezi la kuwalipa linaendelea.

Aidha, kiasi cha shilingi 478,214,660 kimepokelewa kwa ajili ya kutekeleza miradi ya kutoa ajira za muda mfupi (PWP), ambapo kiasi cha shilingi 70,140,700.00 zimetumika na kuongeza kuwa hadi Aprili 2018 kiasi cha shilingi 191,742,860.00 hazijatumika.

Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) unatoa huduma katika vijiji vipatavyo 56 vilivyomo katika mpango wa TASAF III, ambapo vijiji 42 vitapata ruzuku ya malipo kwa walengwa na vijiji 14 vinatarajiwa kuwa katika kundi la utafiti.

Post a Comment

0 Comments