habari Mpya


Hali hii ya Uchafu Soko la Kabwigwa,Kibondo inatishia Afya ya Wananchi.

Tangu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Dkt. John Pombe Magufuli aingie madarakani miongoni mwa mambo aliyoanza nayo akiwashirikisha watendaji wake ni usafi wa miji lakini kwa kuanzia familia.


Alielekeza kila Mkoa na Wilaya  hapa nchini  kuwa na siku ya usafi kwa kila wiki na Jumamosi ya mwisho wa mwezi Nchi nzima kufanya tathimini ya ukaguzi wa usafi katika mazingira na kwamba atakayezembea kufanya na kuhimiza usafi atozwe faini kwa mujibu wa kanuni za kuhifadhi mazingira.

Mikakati hiyo iliwekwa na kila kiongozi au mtendaji akaahidi kutekeleza lakini kwa wilaya ya Kibondo mkoani Kigoma ni tofauti kama kamera yetu ilivyoona kwenye soko la wakulima la Kabwigwa usafi haufanyiki ipasavyo na kuhatarisha wakazi wa eneo hilo kiafya.Baadhi ya watu waliohojiwa wamesema ni jukumu la halmashauri kujenga kizimba na kuzoa uchafu huo hadi nje ya eneo hilo kuwaepusha na magonjwa ya mlipuko kama  kipindupindu na maradhi yatokanayo na uchafu


Nimepita tu na kuelekea mitaaa mingine nashauri tu mamlaka zinazohusika tembelea soko hilo kiafya ni hatari wakati wananchi wakihitaji kupata huduma , kwanza haliko kwenye viwango lakini halmashauri bado inawatoza ushuru kujiongezea mapato ya ndani. 

Picha Na Shaaban Ndyamukama RADIO KWIZERA.


Post a Comment

0 Comments