habari Mpya


DC Muleba Atoa Siku 14 tu kwa Uongozi wa Kata ya Kasharunga Kuboresha Mazingira ya Kituo cha Afya cha Kimeya.

Mkuu wa Wilaya ya Muleba Mkoani Kagera Mhandisi Richard Ruyango ametoa siku 14 tu kwa viongozi wa Kata ya Kasharunga  wilayani humo kuhakikisha wanasimamia kikamilifu ujenzi wa nyumba za watumishi katika kituo cha Afya cha Kimeya ili zikamilike kwa wakati.

 Mhandisi Ruyango amesema hayo mara baada ya kutembelea kituo hicho hapo May 19, 2018 na kukagua ujenzi wa nyumba za watumishi ambapo Serikali imetoa shilingi milioni 400 kwa ajili ya kuboresha kituo hicho ikiwemo vyoo vya kisasa na vyumba za watumishi.


 Aidha amewataka kujenga majengo yenye ubora na sio kuharibu fedha za Serikali kwani endapo ujenzi huo utafanyika kimakosa Mhandisi wa wilaya hiyo atawajibika kutokana uzembe wa kazi yake.


Kwa upande wake Diwani wa kata ya Kasharunga Bw Halidi Husein amemwakikishia mkuu wa wilaya hiyo kuwa ujenzi huo utakamilika kwa wakati na kwa kiwango kikubwa licha ya kuwa na changamoto ya baadhi ya vifaa na vitendea kazi kwenye ujenzi huo.

 Mkuu wa Wilaya ya Muleba Mkoani Kagera Mhandisi Richard Ruyango akikagua ujenzi unaoendelea katika kituo cha Afya cha Kimeya wilayani humo.


 Mkuu wa Wilaya ya Muleba Mkoani Kagera Mhandisi Richard Ruyango akikagua ujenzi unaoendelea katika kituo cha Afya cha Kimeya wilayani humo.

Picha /Habari Na Shafiru Yusuf -Radio Kwizera Muleba.


Post a Comment

0 Comments