habari Mpya


DC Atoa Siku 90 hataki Kaya kukosa Choo.

 Wananchi wakimsikiliza Mkuu wa wilaya ya Uvinza katika mkutano wa Hadhara.

Picha/Habari Na Adrian Eustus -RADIO KWIZERA -Kigoma.

Mkuu wa Wilaya ya Uvinza mkoani Kigoma Bi.Mwanamvua Mlindoko ametoa miezi mitatu kwa Wananchi wa wilaya hiyo ambao hawana Vyoo na kujisaidia Kusikojulikana kuhakikisha wanachimba na kutumia vyoo hivyo.

 Bi.Mlindoko (pichani)ametoa agizo Hilo katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha Mlela Kata ya Kandaga ukilenga kujadili mambo mbalimbali ya kimaendeleo na kwamba baada ya siku 90 hizo kukamilika kamati ya ulinzi na usalama kwa kushirikiana na idara ya afya wilayani humo watapita nyumba kwa nyumba kukagua Kaya ambazo hazina vyoo na kuwachukulia hatua watakaobainika kukosa Choo cha kujisaidia.


 Kwa upande wake Afisa wa Afya wilayani Uvinza Bw. Rajabu Katole amesema ukosefu wa Choo cha kujisaidia ni chanzo kukubwa kinachopelekea magonjwa ya mlipuko ukiwemo ugonjwa wa kipindipindu ambao umekuwa ukijitokeza katika baadhi ya vijijji vya wilaya hiyo na hivyo kila Mwananchi kutakiwa kuchimba Choo na kukitumia pamoja na kuzingatia ushauri wa wataalamu wa afya waliopo.
Post a Comment

0 Comments