
![]() |
Wakizungumza
na Radio Kwizera baadhi yao Mashashi Mwenda, Pendo Makoye na Leonard
Malimi wamesema kutokana na mvua
iliyonyesha hivi karibuni katika kata hiyo ilisababisha daraja hilo kukatika na
kukata mawasiliano baada ya daraja hilo kusombwa na maji hali ambayo imesababisha bei ya soda 1 kupanda
kufikia sh.700 huku bei ya usafiri ikifikia shilingi elfu 6 badala ya shilingi
elfu 3 kufika makao makuu ya wilaya hiyo.
Hata hivyo
wameiomba Serikali kuwatengenezea barabara hiyo ili kurahisisha shughuli za
usafirishaji wa bidhaa kuzifikisha katika soko la BULEGA lililopo katika kata hiyo.
|
![]() |
Mbunge
wa Jimbo la Bukombe MHE. DOTTO MASHAKA
BITEKO amewataka Wananchi kuwa wavumilivu na kwamba amefanya mazungumzo na kampuni ya ujenzi wa barabara STRABAG iliyopo wilayani humo kwa lengo
la kuwasaidia wananchi kuwatengenezea barabara hiyo na kwamba tayari wamekwisha
kufika eneo hilo kwa ajiri ya utafiti wa awali kabla ya kuanza ujenzi.
|
0 Comments