habari Mpya


Askofu Severin Niwemugizi azindua Kanisa la Mtakatifu Paulo Kigango cha Kasuno-Biharamulo.

Askofu wa Kanisa Katoriki jimbo la Rulenge Ngara Askofu Severin Niwemugizi amezindua Kanisa la Mtakatifu Paulo Kigango cha Kasuno Parokia ya Katoke lililogharimu zaidi ya shilingi milioni 12 mpaka kukamilika kwake.

 Shughuli hiyo ya uzinduzi imefanyika hapo May 25, 2018 kijijini Kasuno ambapo Baba Askofu anaendelea na ziara yake ya ukaguzi mbali mbali wa shughuli za maendeleo katika parokia ya katoke shughuli ambazo zinaenda sambamba na uwekaji wa jiwe la msingi pamoja na uzinduzi wa makanisa mbali mbali.

Na James Jovin -Radio Kwizera Biharamulo.

Mhashamu Askofu Severin Niwemugizi amewapongeza waumini wa kanisa la mtakatifu Paulo Kasuno kwa kushiriki pamoja kwa umoja na kuweza kujenga kanisa zuri kwani ni hatua kubwa ukilinganisha na kanisa la lililojengwa kwa nyasi walilokuwa wakitumia zamani.

 
 
Awali Katibu wa Kigango cha Kasuno Bw. Rucas Raulent akisoma lisara mbele ya baba askofu amesema kuwa ujenzi wa kanisa hilo lililogharimu zaidi ya milioni 12 umetokana na michango ya waumini wa kanisa hilo waliojitolea pia nguvu kazi kama kusomba mawe,kokoto na matofari.  
  
kwa upande wao waumini wa Kanisa Katoriki la Mtakatifu Paulo Kigango cha Kasuno wamepongeza ujio wa Baba Askofu na kwamba ujio huo utaongeza hamasa kwa waumini hata ambao walikuwa wamekuwa wapagani.

Post a Comment

0 Comments