habari


Wilaya ya Ngara yaungwa Katika Gridi ya Taifa.


20160922_113854%25281%2529
Taswira Picha ya Mashine / Mitambo ya Tanesco Ngara mkoani Kagera inayozalisha umeme wa megawati 2.5 utakaotosheleza mahitaji   kwa Wakazi wa wilaya hiyo ambapo kila mashine  inazalisha umeme wa kilowati 1250 ambako kwa sasa zimesimama baada ya wilaya ya Ngara mkoani Kagera kuungwa Grid ya Taifa.
20160922_113653
20160922_113610
Shirika la ugavi wa nishati ya Umeme Nchini TANESCO limeiunganisha wilaya ya Ngara mkoani Kagera katika Grid ya Taifa na kubadili mfumo wa uendeshaji kutoka matumizi ya mashine za dizeli kwenda Umeme wa kawaida.

Akizungumza katika uzinduzi wa kuunganishwa katika Gridi ya Taifa wilayani Ngara, Waziri wa Nishati Dkt.Medard Kalemani ameeleza kuwa hatua hiyo itachochea kasi ya maendeleo ya viwanda na kuondokana na Matumizi ya mafuta ya dizeli ambayo yanagarimu kiasi cha shilingi Milioni 236 kila mwezi sawa na  na bilioni 2.83 kwa mwaka.
20160922_114749
Dkt.Kalemani amesema wilaya hiyo imeunganishwa katika Gridi ya Taifa hali itakayopunguza matumizi makubwa ya fedha za serikali katika uendeshaji wa mitambo baada ya kuwa katika matumizi ya mashine zinazotumia dizeli tangu mwaka 2004.

Katika taarifa ya mkoa mkoa wa Kagera kuhusu hali ya nishati ya umeme,Meneja wa TANESCO mkoani humo Mhandisi Francis Maze amesema mapato ya shirika hilo kwa mwaka ni shilingi milioni 500 tu,wakati matumizi kwa mwezi ni  kiasi cha shilingi Milioni 236 sawa na  shilingi bilioni 2.83 kwa mwaka hali ambayo inakwamisha shughuli nyingi za shirika hilo.       

Post a Comment