habari


Wawili Wafariki kwa Ajali ya Basi ,Muleba mkoani Kagera.

Na Shaaban Ndyamukama.

Watoto wawili wakazi wa kijiji cha Katongo kata ya Rulanda wilaya ya Muleba mkoani Kagera wamefariki papo hapo baada ya kugongwa na basi wakati wakienda kwenye masomo ya dini ya kiislamu (madrasa) katika kijiji hicho.

Afisa mtendaji wa kata ya Rulanda wilayani Muleba Adamu Kamiani aliwataja wanafunzi  waliofariki kuwa  ni Muhajiri Abdul Majid (6) na Abdallah Khalid (7) ambao waligongwa leo April 28, 2018 majira ya saa 2:15 asubuhi wakati basi hilo la Kampuni ya Frester lenye namba za usajili T 720 DEV lililokuwa likitokea Bukoba kuelekea Mwanza likimkwepa  Mwendesha bodaboda na wao kugongwa wakitembea kwa miguu

Kamiani alisema  baada yamajeruhi kuondoshwa kwenye vyuma vya basi hilo walipelekwa  kituo cha Afya Kaigara na hospitali ya Rubya wilayani Muleba kwa matibabu zaidi.
Kwa mujibu wa abiria waliokuwa kwenye basi hilo wamesema, chanzo cha ajali ni dereva wa basi alipokuwa akimkwepa mwendesha bodaboda hivyo kuwaparamia vijana hao na kusababisha basi hilo kupinduka.

Muuguzi wa zamu wa kituo cha afya Kaigara Monica Magesa alisema kwamba walipokelewa majeruhi 20 huku wengine saba waliokuwa na hali mbaya walipelekwa Hospitality ya Rubya kwa matibabu zaidi.

Kamanda wa Jeshi la polisi mkoani Kagera Agustino Olomi limefika eneo la alithibitisha vifo vya wanafunzi hao na kwamba jeshi hilo limamshikilia dreva wa basi Mohammed Jafari (49) huku likiendelea kufanya uchunguzi

Kamanda Olomi amewataka  Madereva  kuwa makini wakati huu wa mvua na kuacha kwenda  mwendo kasi unaowafanya  kuvunja sheria za usalama barabarani lazima  wafuate utaratibu

Post a Comment