habari Mpya


Viongozi wa Kuchaguliwa Lawamani Sengerema kwa Kushindwa kukarabati Barabara za Mitaa.

Hali ya barabara zikiwa na hali Mbaya baada ya kuathiriwa na Mvua Katika mji wa Sengerema mkoani Mwanza- Picha/Habari na Erick Ezekiel –Radio Kwizera,Sengerema.
Kutoka na hali hiyo ya Ubovu wa Barabara ,Wananchi wa wilayani hiyo ya Sengerema mkoani Mwanza wametupa lawama zao kwa Viongozi waliowachagua kwa kushindwa kukarabati barabara za mitaa na kusababisha barabara hizo kushindwa kupitika msimu huu wa mvua

Wakizungumza katika stendi ya magari madogo  ya mwembe yanga mjini Sengerema, baadhi ya madereva na watumiaji wa barabara wamesema kwa sasa hali ya usafiri na usafirishaji imekuwa ngumu kutokana na barabara nyingi kugeuka madimbwi ya maji.
Wamesema kuwa licha ya Viongozi waliowachagua kuwapa ahadi nzuri za kukarabati barabara wakati wa kuomba kura, hali imekuwa tofauti ambapo kwa sasa wanasingizia mvua kukwamisha zoezi la ukarabati wa barabara hizo.

Kufuatia hali hiyo, Madereva wa magari ya Umma mjini Sengerema wametishia kugoma kusafirisha abiria siku ya Jumamosi April 21,2018 wakiishinikiza serikali kuboresha barabara ili ziweze kupitika.

Post a Comment

0 Comments