habari


Unit 204 za Damu zapatikana Baada ya Wananchi kujitolea kuchangia Mjini Ngara,Kagera.

Mifuko ya Damu-Picha na Maktaba.

 Jumla ya Unit 204 za damu zimepatikana kutoka kwa Wananchi wakati wa zoezi la uzinduzi wa Kampeni ya kuhamasisha Watanzania kuchangia damu kwa hiari April 7,2018 kwenye Viwanja vya Kokoto katika wilaya ya Ngara mkoani Kagera.

 Mratibu wa Damu Salama  wilayani Ngara, Mugisha Lubagola ametoa taarifa hizo leo Aprili 9,2018 Kupitia Kipindi cha Asubuhi Njema cha Radio Kwizera baada ya zoezi hilo kufanyika katika viwanja vya kokoto ambapo uhamasishaji wa kuchangia damu umefanywa na Radio Kwizera ya mjini Ngara kupitia Kampeni hiyo iliyopewa Jina la DAMU YAKO,MAISHA YANGU na itadumu kwa miezi 6 na itafanyika mkoa wa Kigoma na Kagera kwenye wilaya zote.  

Lubagola amesema  damu hiyo itasaidia wagonjwa wanaopata ajali, watoto wachanga, na akina mama wanaojifungua wakiwemo wa upasuaji katika hospitali na vituo vya Afya wilayani Ngara.
Mwananchi wa mjini Ngara mkoani Kagera akishiriki kuchangia Damu  wakati wa zoezi la uzinduzi wa Kampeni ya kuhamasisha Watanzania kuchangia damu April 7,2018.

 Wilaya ya Ngara huhitaji Unit  290 kila mwezi lakini zinazopatikana kwa watu kuchangia damu ni kati ya  lita 70 mpaka 85.

 Kwa mujibu wa Lubagola amebainisha kuwa  Binadamu ili amchangie mwenzake damu lazima awe na umri wa miaka 18 mpaka 65 na achangie kila baada ya miezi mitatu, awe na afya bila kuwa na magonjwa kama kisukari ambapo siku ya kutoa damu asiwe na ugonjwa wa shinikizo la damu (presha).

Post a Comment

0 Comments