habari Mpya


Unit 164 za Damu zakusanywa Mjini Ngara wakati wa Kampeni ya Damu yako,Maisha yangu ya Radio Kwizera FM.

Mmoja wa Mwananchi wa mjini Ngara mkoani Kagera akishiriki kuchangia Damu  wakati wa zoezi la uzinduzi wa Kampeni ya kuhamasisha Watanzania kuchangia damu April 7,2018 kwenye Viwanja vya Kokoto na inaratibiwa na Kituo cha Radio Kwizera FM cha wilayani Ngara kupitia kipindi chake cha ASUBUHI NJEMA ikishirikiana na na Kamati ya Damu Salama mkoa wa Kagera na Kigoma.

Kampeni hiyo iliyopewa Jina la MAISHA YANGU,DAMU YANGU itadumu kwa miezi 6 na itafanyika mkoa wa Kigoma na Kagera kwenye wilaya zote.


Zoezi hilo liliwakusanya Wananchi mbalimbali katika mjini wa Ngara na Chupa ( Unit )  164 za damu zimekusanywa.
Picha Juu na Chini ni Taswira Picha ya Wanangara walipojitokeza kuchangia damu kwa hiyari  kwenye viwanja vya Kokoto  April 7,2018 wakati wa zoezi la uzinduzi wa Kampeni ya kuhamasisha Watanzania kuchangia damu inayoratibiwa na Kituo cha Radio Kwizera FM cha wilayani Ngara kupitia kipindi chake cha ASUBUHI NJEMA ikishirikiana na na Kamati ya Damu Salama mkoa wa Kagera na Kigoma.
Zoezi la uzinduzi wa Kampeni ya kuhamasisha Watanzania kuchangia damu kwa hiyari wilayani Ngara mkoani Kagera lilipambwa na burudani ya kila aina ikiwemo mchezo wa soka.

Aidha  Kituo cha Radio Kwizera FM cha wilayani Ngara kimeandaa Kampeni hiyo yenye Jina DAMU YAKO,MAISHA YANGU kupitia kipindi chake cha ASUBUHI NJEMA ikishirikiana na na Kamati ya Damu Salama mkoa wa Kagera na Kigoma.


Mchezo wa Soka ,Kumuyange FC walipambana kwenye uwanja wa Kokoto na Murusagamba FC na kutoka sare ya bao 1-1 wakati wa zoezi la uzinduzi wa Kampeni ya kuhamasisha Watanzania kuchangia damu inayoratibiwa na Kituo cha Radio Kwizera FM cha wilayani Ngara.

Post a Comment

0 Comments