habari Mpya


NESCH MINTEC Yaelimisha Wachimbaji wa Madini kufanya Kazi Kisasa.

Wito umetolewa kwa wachimbaji na wafanya biashara ya madini aina ya dhahabu kujenga tabia ya kutumia Maabara za Kisasa kupima madini hayo kabla ya kuyauza ili kuepuka upoteaji.

 Mkurugenzi wa NESCH MINTEC Bw.Happines Nesvinga amesema kuwa wachimbaji wa madini wamekuwa wakiendesha shughuli zao kienyeji hali inayowakosesha mapato na kupeleka kufanya kazi kwa hasara.

Mkurugenzi wa Kampuni ya NESCH MINTEC TANZANIA LIMITED ambao ni wataalam wa madini aina zote katika mkutano wao na wadau wa Madini Kanda ya Ziwa uliofanyika  Jijini Mwanza,akieleza jambo.

Nao baadhi ya Wachimbaji walioshiriki katika mkutano huo akiwemo Mzee Cosmas Nkayamba mchimbaji wa dhahabu katika kata ya Nyakahula wilayani Biharamulo ammekiri kuwa uchimbaji wa kienyeji unawapa hasara na kuiomba Serikali kuwapatia elimu ili kuboresha shughuli zao.

Post a Comment

0 Comments