habari


Mwenge wa Uhuru unakimbizwa Wilaya ya Ngara mkoani Kagera leo April 14, 2018.

Viongozi mbalimbali wa Wilaya ya Ngara wakiongozwa na Mkuu wa wilaya hiyo wakiwa eneo la uwanja wa Kemikimba Benaco unapopokelewa Mwenge wa Uhuru kutoka wilayani Karagwe mkoani Kagera.Picha na Shaban Ndyamukama -Radio Kwizera Ngara.

Mwenge wa Uhuru 2018 unaendelea na mbio zake Mkoani Kagera ambapo tayari Mwenge huo umekimbizwa katika Halmashauri 8 za Muleba, Bukoba, Bukoba Manispaa, Missenyi , Kyerwa ,Karagwe na sasa wilaya ya Ngara leo April 14,2018 ikiwa ni kati ya Halmashauri 9 za Mkoa wa Kagera.

Aidha, tayari miradi zaidi ya 44 yenye thamani ya zaidi ya shilingi 6,309,492,560.70 imetembelewa, kukaguliwa, kuzinduliwa na kuwekewa mawe ya msingi.

Miradi hiyo 44 ni kati ya miradi 65 ya mkoa mzima wa Kagera itakayopitiwa na Mwenge Uhuru wa mwaka huu 2018 yenye Thamani ya shilingi bilioni 12,385,330,354 za miradi yote katika Mkoa kwenye Halmashauri za Wilaya.

Mapokezi Uwanja wa Kemikimba Benaco.

Mwenge wa Uhuru ulipokelewa Mkoani Kagera Aprili 8, 2018 na tayari umekimbizwa katika Halmashauri za Wilaya za Muleba, Bukoba, Bukoba Manispaa, Missenyi, Kyerwa ,Karagwe na sasa unakimbizwa Wilayani Ngara leo April 14, 2018.

Aidha, Mwenge wa Uhuru unatarajiwa kukimbizwa kesho April 15, 2018 katika Halmashur  ya Biharamulo na utakabidhiwa Mkoa wa Kigoma tarehe 16 Aprili, 2018.
Akito ujumbe wa Mwenge wa Uhuru mwaka huu 2018 Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa Charles F. Kabeho katika Halamashauri za Wilaya ambazo tayari zimepitiwa na Mwenge wa Uhuru aliwasistiza Wananchi kuwekeza katika Elimu kwa watoto wao ili kuhakikisha watoto hao wanapata Elimu bora kwa manuaa ya taifa na mkoa wa Kagera hapo baadae.

Kiongozi huyo wa Mbio za Mwenge aliongeza kuwa wazazi wanatakiwa kuhakikisha watoto wao wanapata chakula shuleni kulingana na Waraka wa Serikali unavyoelekeza.

Pia Wazazi wanatakiwa kuwanunulia watoto wao sare za shule, kuwalipia nauli za kwenda shule na kuhakikisha watoto wana vifaa vyote vya shule kama madaftari na kalamu.

Katika Hatua nyingine Kiongozi wa Mbio za Mwenge aliwasisitiza wananchi wa mkoa wa Kagera kuachana na upikaji wa gongo na kusisitiza kuwa gongo ni mojawapo ya dawa za kulevya ambazo hazistahili kutumika katika jamii.

Post a Comment