habari Mpya

Mvua yaleta Maafa wilayani Muleba Mkoani Kagera.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Muleba,Mkoani Kagera Ndg Emmanuel Sherembi, ametembelea na kukagua maeneo na makazi ya watu katika kata ya Karambi yaliyopata maafa kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha ambapo nyumba 45 zimebomoka kuta na nyumba moja imeanguka.

Barabara ya Rugasha,Nyakagoma na Kanyabwenda imemomonyoka, Daraja la Nyakagoma,Rugasha limebomoka, ukuta wa darasa la Shule ya Msingi Nyakagoma umeanguka na mazao yamesombwa na maji.

Habari/Picha na Lucy Binamungu -Afisa Habari Muleba DC.Muoneknao wa Daraja la Nyakagoma,Rugasha likiwa limebomoka.Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Muleba,mkoani Kagera Ndg Emmanuel Sherembi, akitazama ukuta wa Darasa la Shule ya Msingi Nyakagoma ulioanguka kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha ambapo nyumba 45 zimebomoka kuta na nyumba moja imeanguka.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Muleba,Mkoani Kagera Ndg Emmanuel Sherembi, ametembelea na kukagua maeneo na makazi ya watu katika kata ya Karambi yaliyopata maafa kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha ambapo nyumba 45 zimebomoka kuta na nyumba moja imeanguka.

Barabara ya Rugasha,Nyakagoma na Kanyabwenda imemomonyoka, Daraja la Nyakagoma,Rugasha limebomoka, ukuta wa darasa la Shule ya Msingi Nyakagoma umeanguka na mazao yamesombwa na maji.

Post a Comment

0 Comments