habari Mpya


Misenyi Kuanza Chanjo ya Saratani ya Shingo ya Kizazi April 23,2018.

Mratibu wa Huduma ya Chanjo katika  wilaya ya Misenyi Mkoani Kagera Bw Edward  Kagari akizumza na radio Kwizera  juu maandalizi  ya uzinduzi wa chanjo ya saratani ya  mlango wa  shingo  ya kizazi Utaohusisha Wanafunzi na Watoto wa kike wenye umri wa miaka 14 na kuendelea.

Na Wiliam Mpanju-Radio Kwizera Misenyi.

Halmashauri ya wilaya  ya Misenyi mkoani Kagera kupitia  idara  ya afya  inatarajia  kutoa chanjo ya mlango wa  shingo ya kizazi kwa  watoto wa jinsia ya kike wenye  umri wa  miaka 14 na kuendelea, uzinduzi ambao  utafanyika  Kitaifa  na wilaya ya  Misenyi  litafanyika  April 23   hadi 30,2018 katika  shule ya Sekondari  Bunazi.

Aidha Serikali ya Tanzania imezindua kampeni ya chanjo ya kuzuia saratani ya shingo ya kizazi na zaidi ya wasichana laki 6 walio na umri kati ya miaka 9 hadi 14 watachanjwa nchini nzima.

Saratani ya shingo ya kizazi ni saratani ambayo hutokea kwenye shingo ya kizazi cha mwanamke - ambayo ni kiingilio kutoka uke hadi katika mfuko wa uzazi.

 Ni moja kati ya zaidi ya aina 100 ya virusi vya human papilloma (HPV), ambavyo 13 vinasababisha saratani.

Pia aina fulani ya HPV vinaambukizwa kwa njia ya ngono.

 Baadhi ya sababu za kupata ugonjwa huo ni kushiriki ngono ukiwa na umri mdogo, ukifanya ngono na washiriki wengi , kuvuta sigara na kuwa na virusi vya Ukimwi.
 
Dalili ni

 > kupata hedhi kwa mzunguko usio wa kawaida au kutoka damu baada ya kujamiana

> maumivu ya mgongo, mguu na fupanyonga

> uchovu, kupungua kwa uzito na kutokuwa na hamu ya kula

>maumivu kwenye uke au kutoa harufu mbaya

>kuvimba kwa mguu mmoja

Uchunguzi wa virusi hivyo unastahili kufanyika ili kuvigundua mapema. Chanjo za HPV ni hatua nyingine ya kuziuzi.

Matibabu kwa wagonjwa walio na virusi hivyo yanategemea na viwango vya virusi hivyo mwilini, hata hivyo yanaweza hitaji kutibiwa kwa njia ya upasuaji na kutoa sehemu au mfuko wa uzazi mzima au kutumia miyonzi.


Chanzo: Shirika la Afya duniani.

Post a Comment

0 Comments