habari


Miongoni mwa Habari zilizosikika Saa 24 zilizopita Radio Kwizera FM.

Mkurugenzi  wa NESCHMINTEC Bw.Happines Nesvinga .Picha kutoka Maktaba yetu.

Source; RK, OM (mwenge)

Ed: FM

Date: Tuesday, April 17, 2018KIBONDO

Mkimbiza mwenge kitaifa Bw Charles Kabeho amemuagiza mkuu wa Wilaya ya Kibondo kwa kushirikiana na mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya hiyo kutafuta namna ya kutatua changamoto ya wanafunzi wa shule za msingi kutokuwa na sare kamili za shule

 Bw Kabeho ametoa agizo hilo leo akitoa ujumbe wa mwenge wakati wa makabidhiano ya mwenge wa uhuru kijiji cha Kumkugwa kata ya Misezero ukitokea Wilaya ya Kakonko na kuanza mbio zake wilayani ya Kibondo

Amesema amebaini watoto wengi wa shule za Msingi kwenye maeneo ya wilaya ya Kibondo hawana sare kamili za shule pamoja na kutokua na viatu hivyo mkurugenz na mkuu wa wilaya watazame namna ya kushirikiana na wazazi kuhakikisha wanapata sare kamili 

Kwa upande wake mkuu wa Wilaya ya Kibondo Bw Louis Bura ameahidi kuyafanyia kazi maagizo hayo na kuhakikisha watoto hao wanakua na sare kamili pamoja na viatu nasio ndala au yeboyebo


Source; RK, AK (sumu)

Ed: FM

Date: Tuesday, April 17, 2018BUKOBA

Watu 3 wakazi wa kata ya Miembeni manispaa ya Bukoba Mkoani Kagera wamelazwa katika hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Kagera baada ya kula chakula kinachodhani kuwa na sumu

Kamanda wa jeshi la polisi Mkoani Kagera Agustino Olomi amesema watu hao  ni wafanyakazi wa nyumba ya kulala wageni ya Lilly Vila ambapo April 15 mwaka huu walimpokea mteja aliewapatia kitu kinachodhaniwa kuwa ni pipi yenye sumu na kupelekea kupoteza fahamu

Amesema watu hao ni pamoja na mlinzi wa nyumba hiyo ya wageni Mwemezi Erasto, Wafanyakazi 2 wa kike ambao majina yao hayajajulikana na kwamba mtu huyo alifanya wizi wa fedha ambazo hazijajulikana kiasi chake pamoja na vifaa mbalimbali katika nyumba hiyo

Insert……….Agustino Olomi
Cue in…….
Cue out…….

Kwa upande wao baadhi ya wakazi walioshuhudia watu hao wamesema walikuwa na hali mbaya kwani walikuwa hawajitambui na kwamba wangecheleweshwa kufikishwa hospitali kupata huduma watu hao wangepoteza maisha 

Source; RK, EE (ushauri)

Ed: AG

Date: Tuesday, April 17, 2018SENGEREMA

Viongozi waliochaguliwa na wananchi wametakiwa kuacha tabia ya    kukarabati barabara pale wanaposikia ujio wa viongozi wa kitaifa katika maeneo yao kwa ajili ya kukwepa aibu mbele ya viongozi hao  

Ushauri huo umetolewa na Diwani wa kata ya Nyampulukano wilayani Sengerema mkoani Mwanza kupitia CHADEMA Bw. Emmanuel Zacharia wakati akizungumza na redio kwizera kufuatia barabara nyingi katika halimashauri hiyo kupitika kwa shida nyakati za mvua

Bw. Zacharia amesema kuwa baadhi ya viongozi wamejijengea desturi ya kukarabati barabara katika maeneo yao pindi wanapotembelewa na viongozi wa kitaifa ambapo hali hiyo inadidimiza maendeleo ya wananchi   waliowachagua

Insert…..Zacharia
Cue in…
Cue out…

Kadhalika diwani Emmanuel Zacharia amesema kuwa huu si wakati wa vyama kundelea kulumbana, badala yake watumie fursa waliyonayo   kuwatumikia wananchi kama walivyoahidi wakati wakiomba ridhaa ya kuwaongoza


Source; RK, wm (mnyama)

Ed: AG

Date: Tuesday, April 17, 2018MISSENYI

Wakazi wa kijiji cha Kashaba kata ya Kyaka wilayani Missenyi mkoani Kagera wameingiwa na hofu kufuatia taarifa za kuingia mnyama anayesadikiwa kuwa Fisi ambaye anadaiwa kuuwa mbuzi wanne na kondoo mmoja

Wakazi hao wameiambia redio Kwizera kuwa fisi huyo amekuwa akivamia nyumba za watu majira ya usiku na kuanza kushambulia mifugo na kuiua 

Pia wameeleza kwamba kutokana na hofu iliyopo kwa sasa, baadhi ya wanafunzi wanashindwa kwenda shule na wanawake kwenda kuchota maji hivyo wanaiomba halmashauri isaidie kumtafuta mnyama huyo ili waweze kumuua

Insert…Wananchi
Cue in ….
Cue out …..

Kaimu mkurugenzi wa halmshauri ya Wilaya ya Missenyi Bw. James  Matekele amesema wameshapata  taarifa za kuwepo kwa mnyama huyo na tayari ameagiza wataalam wa idara ya wanyama pori kwenda katika kijiji hicho cha Kashaba ili kujua kama ni Fisi au Chui waweze kumpiga risasi  huku akiwataka wananchi kuwa watulivu 


Source; RK, AE (Diwani atuhumiwa kumpiga muuguzi)

Ed: AG

Date: Tuesday, April 17, 2018KIGOMA

Wahudumu wa afya katika zahanati ya Msufini iliyopo kata ya Mwanga kaskazini manispaa ya Kigoma ujiji mkoani Kigoma wamegoma kutoa huduma kwa madai kuwa diwani wa kata hiyo amempiga mmoja wa wauguzi wa zahanati hiyo na kusababisha baadhi ya wagonjwa kuondoka bila kupatiwa matibabu

Tukio hilo limetokea mwishoni mwa wiki iliyopita ambapo muuguzi aliyekutwa na tukio hilo amesema ameshangazwa na kitendo cha diwani kufika na kuleta vurugu katika zahanati hiyo na kusababisha baadhi ya wagonjwa kusambaratika bila kupatiwa matibabu

Insert…………………….Muuguzi wa Zamu
Que in……………………….diwani
Que out………………………kwanza

Akizungumza juu ya tuhuma hizo, diwani wa kata ya Mwanga kaskazini Bw.Revocatus Chiponda amekanusha kuhusika na tukio hilo lakini amedai kupokea malalamiko ya wananchi wake juu ya huduma mbovu zinazotolewa na muuguzi huyo ikiwemo matamshi yasiyorafiki wakati akitoa huduma kwa wagonjwa

Insert…………Revocatus chiponda
Que in…………..nimepokea
Que out……………tutaendelea

Aidha kamanda wa jeshi la Polisi mkoani Kigoma kamishina msaidizi Martin Ottieno amethibitisha kupokea taarifa hizo na kwamba upelelezi zaidi wa tukio hilo unaendelea


Source; RK, JJ (vitambulisho vya ukaazi)

Ed: FM

Date: Tuesday, April 17, 2018BIHARAMULO 

Raia wa nchi za nje wanaoishi Wilayani Biharamulo Mkoani Kagera wametakiwa kuomba upya Hati ya ukaaji ili waweze kuishi kwa kufuata utaratibu wa nchi hii ili kuepuka matatizo yasiyo ya lazima 

Akizungumza na redio kwizera ofisini kwake afisa uhamiaji wa wilaya ya Biharamulo Bw Raulent Mutare amesema tangu mwaka 2016 serikali ilifungua utaratibu wa kutoa hati za ukaaji kwa raia wa kigeni lakini wanaojitokeza kuomba hati hizo ni wachache 

Amesema yeyote anayeishi nchini bila hati hiyo ama kibali chochote anahesabika kama mhamiaji haramu hivyo ni vyema wakafuata utaratibu ili kuweza kuishi kwa amani bila usumbufu wowote 

Amewataka viongozi wa vijiji na kata kutoa taarifa za raia wa kigeni wanaoishin nchini kinyume cha utaratibu ili waweze kuchukuliwa hatua za kisheria kwa manufaa ya usalama wa nchi hasa watu wanaishi nao huko vijijini 

Source; RK, Ak (CHANJO)

Ed: AG

Date: Tuesday, April 17, 2018

BUKOBA

Zaidi ya wasichana elfu 35 na 917 wenye umri wa miaka 14 mkoani Kagera wanatarajiwa kupatiwa chanjo ya kujikinga na saratani ya shingo ya kizazi inayotarajiwa kutolewa na serikali hivi karibuni

Mratibu wa chanjo mkoani Kagera Bw. Deocres Mjwauzi amesema kuwa chanjo hizo zitatolewa kwenye vituo vya kutolea huduma za afya vilivyoko ndani ya mkoa huo, vituo vya mikoba mia 915 na kwenye shule za msingi ambazo zitakuwa katika mazingira magumu kufika katika vituo vya kutolea huduma hiyo

Amesema kuwa serikali imeamua kutoa chanjo hiyo kutokana na tatizo la saratani ya shingo ya kizazi kuonekana kuwa ya kwanza kwa vifo vya wanawake ikifuatiwa na saratani ya matiti na hivyo amewataka wazazi kuhakikisha wanawahamasisha watoto wao kujitokeza kupata chanjo hiyo

Nao baadhi ya wazazi waliozungumza na redio kwizera katika manispaa ya Bukoba wameipongeza serikali kwa kuamua kukabiliana na tatizo la saratani ya kizazi na kwamba wako tayari kuwaruhusu watoto wao kushiriki zoezi hilo 


Source; RK, FB (bunge)

Ed: FM

Date: Tuesday, April 17, 2018DODOMA

Serikali imewataka wananchi Mkoani Kigoma kuendelea kuwa wavumililu katika ujenzi wa barabara unao endelea ili kuunganisha na mikoa mingine nchini

Kauli hiyo imetolewa leo Bungeni mjini Dodoma na naibu waziri wa ujenzi, uchukuzi na mawasiliano Mhandisi Edwin Ngonyani na kusema kuwa kwasasa serikali inaanda pesa kwa ajili ya kumlipa mkandarasi mvua zinapo pungua ujenzi undelee 

Aidha Mhandisi Ngonyani amesema pamoja na kuwa na deni hilo serikali bado inaendelea na jitihada za kuhakikisha mkandarasi analipwa na ujenzi uweze kuendela mara moja

Insert…..WAZIRI
Cue in….
Cue out…

Majibu hayo yanakuja kufuatia mbunge wa Kasulu mjini Bw Daniel Nsanzungwanko kuhoji ujenzi wa bara bara ya Kidahwe Kasulu kilomita 63 umesimama sababu ya mkandarasi kutolipwa pesa yake, nilini atalipwa pesa hizo

Post a Comment