habari Mpya


Miongoni mwa Habari zilizosikika Saa 24 zilizopita Radio Kwizera FM.

Naibu Waziri wa Madini Mhe.Dotto Biteko.

Source; RK, SD (ujenzi)
Ed: FM
Date: Friday, April 13, 2018
KAHAMA

Wizara ya Madini nchini inatarajia kuanza ujenzi kiwanda cha kisasa cha kuchenjua dhahabu ya wachimbaji wadogo katika kijiji cha Katente Wilayani Ushirombo Mkoani Geita ambacho kitakuwa cha kwanza hapa nchini 

Akizungumza na wachimbaji wadogo wa Wilaya ya Kahama, Naibu waziri wa Madini Bw Dotto Biteko amesema kiwanda hicho kinajengwa mwaka huu katika eneo hilo ili kuwapunguzia mzigo wachimbaji 

Amesema viwanda kama hivyo nchini vitajengwa vingine viwili katika maeneo mengine yenye madini ili kuwasidia wachimbaji wadogo kuthamaniwa kuliko hivi sasa

Hata hivyo amewaonya wachimbaji kuwa wazalendo na kuacha tabia ya kutorosha madini ambapo takwimu zinaonyesha wachimbaji wadogo wamezalisha kilo 540 za dhahabu nchini kwa mwaka jambo ambalo sio sahihi


Source; RK, EM (mwenge)
Ed: FM
Date: Friday, April 13, 2018
KARAGWE

Wananchi Wilayani Karagwe Mkoani Kagera wametakiwa kulima ndizi kwa wingi ili kuongeza chakula katika familia zao ikiwa ni pamoja na kujiongezea kipato

Mkimbiza mwenge wa uhuru kitaifa Bw Charles Kabeo amesema hayo baada ya uzinduzi wa shamba la mgomba kwenye kata ya Kituntu Wilayani humo

Aidha Bw Kabeo amesema zipo aina nyingi za migomba ikiwa ni pamoja na ndizi kali zinazotumika kutengenezea gongo ambayo ni jamii ya madawa ya kulevya hivyo amemtaka mkuu wa jeshi la polisi wilayani humo kupiga marufuku aina hii ya migomba

Awali mmiliki wa shamba hilo la mfano katani hapo amesema bado anakabiliwa na ugonjwa wa mnyauko  na ukosefu wa bei za bidhaa yake kitendo kinachosababisha uchumi wake kuyumba 

Source; RK, EE (taka)
Ed: FM
Date: Friday, April 13, 2018
SENGEREMA

Wananchi Wilayani Sengerema Mkoani Mwanza wamegomea zoezi la kuchangia tozo ya taka kwa ajili kulipa wanaofanya usafi katika vizimba vya taka hali inayosababisha kuchelewa kutoa taka zilizojaa vizimbani.

Kauli hiyo imetolewa na mkuu wa Wilaya ya Sengerema  Bw Emmanuel Kipole ambapo amesema kila kaya inatakiwa   kuchangia shilingi elfu moja  ambapo kwa wafanyabiashara ni shilingi elfu 3  kila mwezi kwa ajili ya kuwalipa wanaofanya usafi 

Insert.... Kipole
Cue in...
Cue out... 


Nao baadhi ya wananchi waliotoa tozo hiyo wamesema licha ya   kuchangia fedha hizo bado mamalaka husika inashindwa kuondoa taka kwa wakati kwa baadhi ya maeneo
Kwa upande wake  mkuu wa idara  ya usafi na Mazingira wa Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema Bw Ally Salim  amesema sababu inayowafanya kuchelewa kuondoa taka kwa wakati kwa sasa  ni   mvua zinazoendelea kunyesha 
Insert.... Afisa mazingira

Cue in….
Cue out…  

Source; RK, GM (mikopo)
Ed: FM
Date: Friday, April 13, 2018
GEITA
Halmashauri ya mji wa Geita imetoa kiasi cha shillingi milioni 65 za mkopo kwa vikundi 14 vya vijana na wanawake ili kuboresha shughuli za vikundi hivyo vyenye lengo la kuanzisha viwanda vidogo vidogo na utunzaji wa mazingira
Akizungumza katika mafunzo ya wajasiriamali  yaliyoandaliwa na halmashauri hiyo kwa kushirikiana na shirika la SIDO Mkoani Geita, Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri  Bw Modest Aprinary amesema fedha hizo zimetolewa ili kuviwezesha vikundi hivyo kuanzisha viwanda vidogovidogo kuiwezesha serikali kufikia uchumi wa kati
Aidha amevitaka vikundi hivyo kutumia fedha zilizotolewa kulingana na makubaliano yao, na kurejesha mikopo hiyo kwa wakati ili fedha hizo ziendelee kusaidia vikundi vingine vinavyoendelea kuanzishwa Wilayani humo
Insert……….Aprinary
Cue in…
Cue out…
Aidha meneja wa SIDO Mkoa wa Geita Bw Jalphary Donge amewataka washiriki wote wa mafunzo hayo kutumia elimu waliyoipata kwa kila hatua ili kuboresha bidhaa zao ili waweze kunufaika na vikundi hivyo.

Post a Comment

0 Comments