habari


Matukio Picha ya Mbio za Mwenge wa Uhuru wilayani Ngara Leo April 14,2018.

Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Charles Kabeho akiongoza mchakamchaka wakuukimbiza Mwenge huo hapa wilayani Ngara unaokimbizwa baada ya kuwasili na kuzindua mradi wa ujenzi wa barabara za mitaa kwa kiwango cha lami mjini Ngara.

Mwenge wa Uhuru umekimbizwa wilayani Ngara mkoani Kagera leo April 14, 2018 na kesho April 15,2018 utakabidhiwa wilayani Biharamulo katika Kata ya Nyakahura kuendelea na mbio zake mkoani Kagera kabla ya April 16,2018 kuingia mkoani Kigoma. -Picha na Shaaban Ndyamukama –Radio Kwizera Ngara.

Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Charles Kabeho akiongoza mchakamchaka wakuukimbiza Mwenge huo hapa wilayani Ngara unaokimbizwa baada ya kuwasili na kuzindua miradi ya Kielimu ,Maktaba na Maabara pamoja na Bweni la Wanafunzi katika Shule ya New Rusumo Vision English Medium Primary School wilayani Ngara mkoani Kagera leo April 14, 2018. 
Mkuu wa Gereza la Rusumo Wilayani Ngara mkoani Kagera SP Daniel Ndarugilire (kulia) akimkabidhi kiongozi wa mbio za Mwenge kitaifa Charles Kabeho zawadi mkungu wa ndizi leo April 14, 2018 baada ya kuzindua Shamba la Migomba lenye thamani ya Shilingi 8 milioni linalohudumiwa na wafungwa, Kushoto ni mkuu wa wilaya ya Ngara Michael Mtenjele.

Post a Comment