habari


Lipuli FC yaivuta shati Simba SC Ligi Kuu.

Simba SC imepunguzwa kasi baada ya kulazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na wenyeji, Lipuli FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara Uwanja wa Samora mjini Iringa leo April 21, 2018.

Pamoja na sare hiyo, Simba SC inaendelea kuongoza Ligi Kuu, ikifikisha pointi 59 baada ya kucheza mechi ya 25, mbele ya mabingwa watetezi, Yanga SC wenye pointi 47 za mechi 22, wakati Lipuli inafikisha pointi 32 katika mechi ya 26 na kupana kwa nafasi moja kutoka ya nane, ikiishusha Ruvu Shooting.

Katika mchezo huo Lipuli FC ilikuwa ya Kwanza kujipatia goli lilifungwa na Adam Salamba huku Simba SC ikisawazisha goli hilo kupitia kwa Mchezaji wake Laudit Mavugo.

Post a Comment