habari


Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa atekezeta Zana za Uvuvi Haramu wilayani Muleba.

Na Shafiru Yusuf –Radio Kwizera- Muleba.

Zana za uvuvi usiofuata utaratibu zenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 365 zimeteketezwa kwa moto na Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Bw Charles Francis Kabeho katika mwalo wa Magarini uliopo Kata ya Nyakabango Wilayani Muleba Mkoani Kagera.

Akisoma taarifa hiyo Afisa Uvuvi  wilaya ya Muleba mkoani Kagera Bw Maengo Nchumani wakati wa uzinduzi wa jengo la bandari ya kupokelea samaki, amesema kwa kipindi cha miezi saba wamekamata zana za uvuvi usiofata utaratibu zenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 2 na watuhumiwa 86 pamoja na mitumbwi 151.

Amesema pamoja na kukamata zana hizo zenye thamani ya shilingi bilioni moja zimesalimishwa na kuna changamoto ya wavuvi kutoacha uvuvi usiofuata utaratibu na wanashirikiana na kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya hiyo ili kutokomeza Uvuvi usiofata utaratibu.

Kwa upande wake kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa Bw Charles Francis Kabeho amewataka wavuvi kutumia Uvuvi unaofata utaratibu kisheria ili kulinda Rasilimali ya ziwa Victoria.
Aidha Mwenge wa Uhuru umepokelewa April 8, 2018 Mkoani Kagera na Mkuu wa Mkoa Meja Jenerali Mstaafu Salum M. Kijuu kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabrie Luhumbi katika Kijiji cha Nyakabango  mpakani mwa mkoa wa Kagera na Geita.

 Mkoa wa Kagera Mwenge wa Uhuru unapitia Jumla ya miradi 65 yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 12.38.

Katika miradi hiyo 65 Mwenge wa Uhuru Utazindua miradi 33, utakagua miradi 15, Utaweka mawe ya msingi katika miradi 13 pamoja na miradi 19 ambayo itatembelewa na kukaguliwa.

Post a Comment

0 Comments