habari Mpya


Kagoma FC Bingwa Wa Muleba mia mia Cup 2018.

Habari/Picha Na Shafiru Yusuf –Radio Kwizera Muleba.

Timu ya Kagoma FC imeibuka Bingwa wa mashindano ya Muleba mia mia Cup 2018 wilayani Muleba mkoani Kagera baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 3 -2 dhidi ya Timu ya Maduka 9 FC katika mchezo wa fainali ya mashindano hayo iliyofanyika jana April 14, 2018 uwanja wa David Zimbihile mjini Muleba.
Mashabiki na Viongozi mbalimbali na Mashabiki wa Timu ya Kagoma FC na furaha ya Ubingwa.

Kwa ushindi huo Kagoma FC imeondoka na Zawadi ya Kikombe na  kitita cha shilingi milioni tatu huku Maduka 9 FC ikipata shilingi milioni mbili na Katoke FC ikipata shilingi milioni moja.

Post a Comment

0 Comments