habari Mpya


Kagera Sugar,Simba SC na Ruvu Shooting wapeta Ligi Kuu Tanzania Bara.

A
Wachezaji wa Kagera Sugar wakimpongeza mwenzao Japhary Kibaya mara baada ya kuwafungia bao la pili na kufanya matokeo kuwa 2-1 katika mchezo huo wa Ligi Kuu Tanzania Bara leo April 16, 2018 katika uwanja wa kaitaba,Bukoba mkoani Kagera. 
Picha zote na Faustine Ruta – Bukoba.
3
Kikosi cha Timu ya Kagera Sugar  kilichoanza dhidi ya Timu ya Mtibwa Sugar  leo April 16, 2018  na Matokeo hayo yameifanya Kagera Sugar  ifikishe pointi 26 nafasi ya 12 baada ya kucheza mechi 25 za Ligi wakati Ruvu Shooting ikienda nafasi ya 7 ikiwa na pointi 32, imecheza mechi 25.
 
4
Kikosi cha Timu ya Mtibwa Sugar kilichoanza dhidi ya  Kagera Sugar.
1
Kagera Sugar imetumia vyema Uwanja wa nyumbani wa Kaitaba mjini Bukoba mkoani Kagera baada ya kuibuka na ushindi wa magoli 2-1 dhidi ya Mtibwa Sugar.
 
Katika Mchezo huo ulianza kwa kasi, mabao ya Kagera Sugar yote yalifungwa na Jaffar Kibaya dakika za 45 na 53, huku la wageni Mtibwa Sugar likifungwa na Salum Kihimbwa dakika ya 26.

mechi nyingine ni kwa Ruvu Shooting imeibuka na ushindi wa 3-1 ugenini dhidi ya wenyeji, Ndanda FC Uwanja wa Nangwanda Sijaona, Mtwara. 
 

 

Post a Comment

0 Comments