habari


Hii ndo Taswira ya Soko la Bunazi wilayani Misenyi,Kagera.

Mfanyabiashara akiuzaji bidhaa zake chini katika Soko la Bunazi wilayani Missenyi mkoani Kagera kwenye mazingira machafu ya kujaa maji na matope yaliyosababishwa na mvua zikiwazuia wafanyabiashara kuuza baada ya mvua kunyesha zaidi ya masaa manane na bidhaa kusombwa na maji.

Habari/Picha Na Wiliam Mpanju-Radio Kwizera Misenyi.


Wafanyabiashara wa soko la bunazi wakisikitika baada ya bidhaa zao kuchafuliwa na zingine kusombwa na maji kutokana na kuuzia bidhaa hizo chini na kuiomba halmashauri ya wilaya ya Misenyi mkoani Kagera kuwajengea miundombinu rafiki ya wafanyabiasahra ikiwemo chanja au meza za kuuzia.


Afisa Afya na Mazingira wilaya ya Missenyi Bw Ladslaus Owisso akijibu baadhi ya malalamiko ya Wafanyabishara kwa kushindwa kuwajengea miundombinu ya soko iliyorafiki ikiwemo meza,ametoa siku 7 mpaka April 22,2018  kila mfanyabiashara ajenge uchanja au meza  kwa ajili kuuzia bidhaa zake.

Pia amewataka Maafisa Afya na Viongozi wa Soko hilo kusimamia usafi ndani ya soko ikiwemo wafanyabiashara kuuza bidhaa zilizosafi hasazitokazo shambani.

Post a Comment