habari Mpya


DC Ngara – ‘’Saidieni Juhudi za Serikali Kufuta Umaskini katika Kaya Maskini’’.

Mkuu wa wilaya ya Ngara mkoani Kagera Luteni Kanali Michael Mangwela Mtenjele –Habari/Picha na SAMWELI LUKAS –Radio Kwizera Ngara.

Jumla ya wakufunzi 20 wamepatiwa mafunzo ya kuhamasisha wanufaika wa mfuko wa TASAF ili kuunda vikundi vya kuweka na kuwekeza wilayani Ngara mkoani Kagera wametakiwa kutumia elimu hiyo ilikuisaidia wanufaika hao kuondokana na umasikini.

Kauli hiyo imetolewa jana na mkuu wa wilaya ya Ngara mkoani Mkoani Kagera Luteni Kanali Michael Mtenjele katika ufunguzi wa mafunzo kwa timu ya wakufunzi hao ambao wataagizwa kuzungukia vijiji vyote ilikuwaelimisha kaya masikini zilizo katika mpango wa TASAF kujiunga katika vikundi mbali mbali vyakuweka na kuwekeza ilikaya hizi ziondoke katika umaskini.

Luteni Kanali Mtenjele amesema wakufunzi wanapaswa kuwaelimisha walengwa wa mfuko wa TASAF kuhusu hatua zinazotakiwa kufuatwa ilikujiunga katika vikundi na kushiriki katika shughuli zingine za kukuza uchumi wa kaya.

Serikali inamalengo mazuri kuhakikisha kila mtanzania anaishi maisha mazuri ninyi mliochaguliwa kuiwakilisha serikali kwenda kutoa elimu kwa kaya hizi zilizopo katika mfuko wa TASAFU hakikisheni mnafuata maelekezo mnayo pewa ilikuwasaidia wanachi wetu kuondoka katika umasikini” alisema Mtenjele.
Wakufunzi wanao tajia kuwatembelea vijijini wanufaika wa mfuko wa TASAF wakipatiwa elimu na wawezeshaji kutoka jijini Dar es salaam.   

Katika hatua nyingine amesema walengwa wa mfuko  huo watapata ujuzi utakao wasaidia kutekeleza miradi yao kwa faida na hivyo kuongeza kipato na kupunguza umasikini.

Niwaombe wanachi wa Ngara hasa wale waliopo katika mfuko huu wa TASAF elimu hii watakayo ipatiwa na timu ya wakufunzi wetu watakao wafikia vijijini huko ebu waipokee kwani hii ni kwafaida yao wenyewe na maisha yao” alisema Mtenjele. 
Picha Juu na Chini ni Wakufunzi wanao tarajia kuwatembelea vijijini wanufaika wa mfuko wa TASAF wakifuakifutilia kwa ukaribu elimu iliyo kuwa ikitolewa na wawezeshaji kutoka jijini Dar es salaam.

Mkuu wa wilaya ya Ngara mkoani Kagera Luteni Kanali Michael Mangwela Mtenjele akiwa katika picha ya pamoja na wawezeshaji kutoka jijini Dar es salaam katika viti vya mbele huku safu ya nyuma wakiwa ni wakufunzi walio patiwa elimu.

Post a Comment

0 Comments