habari


Abiria wasota siku ya 4 sasa baada ya Maji kukata Barabara eneo la Kazulamwa/Kigoma.

Mamia ya abiria kutoka Jijini Dar es salaam kwenda mjini Kigoma, na kutoka Kigoma kwenda Tabora wamekwama kuendelea na safari zao baada ha magari waliyokuwa wakisafiria kukwama katika pori la Kazulambwa mkoani Tabora baada ya mvua zinazoendelea kunyesha kupelekea maji kujaa na barabara kukatika.

Kwa taarifa zaidi ni kwamba tatizo Hilo lina takribani siku 4 sasa licha ya juhudi zinazoendelea kuhakikisha linatatuliwa na abiria kuendelea na safari zao kama kawaida.

Picha/Habari Na Adrian Yustas Radio Kwizera Kigoma.

Post a Comment